. Rais Xi-Jinping wa China na mwenzake Donald Trump wa marekani |
Utawala wa rais Trump unapanga kutangaza vikwazo dhidi ya China siku ya Alhamisi baada ya kubaini kwamba taifa hilo linashinikiza wizi na uhamisho wa ubunifu kutoka biashara za Marekani.
Ikulu ya whitehouse imesema kuwa hatua hiyo inajiri baada ya miaka kadhaa ya mazungumzo yalioshindwa kupata suluhu kuhusu wala hilo.
Vikwazo hivyo vitashirikisha ushuru na masharti mengine.
Mpango huo umezua hofu kuhusu vita vya kibiashara. Ikulu ya whitehouse iliripotiwa na vyombo vya habari vya Marekani kuweikea ushuru wa kati ya $30bn-$60bn kwa mwaka pamoja na masharti ambayo yatazuia uwekezaji .
Vilevile huenda Marekani ikawasilisha malalamishi yake kwa shirika la biashara duniani WTO, kulingana na maafisa wa biashara.
Mpatanishi mkuu wa biashara nchini Marekani Robert Lighthizer aliambia wabunge wa Congress siku ya Jumatano kwamba Marekani inafaa kuiwekea China shinikizo kali na shinikizo ya chini watumiaji wa Marekani.
Bwana Lighthizer amesema kuwa kulinda ubunifu ni muhimu kwa uchumi wa Marekani.
''Ni swala mushimu sana'' , alisema bwana Lighthizer. ''Nadhani kitakuwa kitu muhimu ambacho kitafanyika katika kuleta usawa wa kibiashara''.
Je nini kilichoshinikiza kuwekwa kwa ushuru huo?
Afisa wa biashara nchini Marekani ambaye alizungumza na wanahabari alisema kuwa Marekani ina ushahidi kwamba China inataka kampuni za Marekani kuingia katika ushirikiano na kampuni za China ili kuingia katika soko la taifa hilo kwa lengo la kuzishinikiza kampuni hizo kuhamisha teknolojia yao
Marekani pia iligundua kwamba China inawekeza katika kampuni muhimu za Marekani na kufanya mashambulio ya mitandao.
Matokeo hayo yanatoka katika uchunguzi ulioagizwa na rais Trump mwezi Agosti kwa jina 301.
Katika kipengee cha 301 cha sheria ya biashara, serikali imejipatia uwezo wa kuwekea vikwazo mataifa ambayo inahisi hayafanyi biashara kwa usawa.
Bwana Trump mara kwa mara amekuwa akilalamika kuhusu ukosefu wa usawa kibiashara kati ya Marekani na China.
Je hatua hiyo inaungwa mkono na wengi?
Kuna wasiwasi mkubwa nchini Marekani kwamba China inatafuta teknolojia ambayo wanaweza kuitumia kijeshi. Bunge la Congress pia linapanga kupitisha sheria ambayo itaipatia serikali uwezo wa kubadilisha mikataba ya biashara za kigeni kutokana na vitisho vya kununua viwanda vya Marekani.
Lakini wanasiasa na viwanda ikiwemo watumiaji wameonyesha wasiwasi kwamba huenda China ikalipiza kisasi.
Bwana Lighthizer amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa China ikalipiza kisasi akidai kwamba Kilimo cha Marekani huenda kikaathiriwa , lakini akasisitiza kwamba hatua hiyo haitaizuia Marekani kuchukua hatua.
Iwapo watalipiza kisasi basi Marekani italazimika kuwalinda wakulima wake.
Je China imesema nini?
China imesema kuwa hakutakuwa na mshindi yeyote katika vita vva kibiashara.
Siku ya Jumanne , siku ya mwisho ya kikao cha kila mwaka cha chama tawala cha taifa hilo, kiongozi wa China Le Keqiang amesema kuwa ombi lake ni kwamba pande zote mbili zinafaa kutulia.
Pia alisema kuwa anatumai kwamba Marekani itapunguza masharti kuhusu bidhaa za kiteknolojia zinazoingia China.
Post a Comment