Jesse Lingard |
Meneja wa Watford Javi Gracia hajui ikiwa kiungo wa kati wa Ufaransa Abdoulaye Doucoure, 25, atasalia Watford licha ya Manchester United, Liverpool, Arsenal na Tottenham kuonyesha nia ya kumsaini (Watford Observer)
Mshambulizi wa Manchester United Jesse Lingard, 25, atapata mkataba mpya huko Old Trafford miezi 11 baada ya kusaini mkatataba ulioboreshwa. (Sunday Star)
Luis Enrique |
Kiungo wa kati wa Bournemouth Harry Arter ameachwa nje ya mechi sita za klabu hiyo. Mchezaji huyo wa miaka 28 hivi majuzi ameh amehusishwa na kuhamia West Ham. (Bournemouth Echo)
Chelsea watahitaji kumenyana na Paris St-Germain ikiwa wangetaka kumfanya meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique kuwa meneja wao.
Sam Allardyc |
Meneja wa Huddersfield Town David Wagner ameibuka kuwa windo la Borussia Dortmund. (Sunday People)
Meneja wa Everton Sam Allardyce anaamini kuwa mshambulizi wa Uturuki Cenk Tosun, 26 ameanza kulipa pauni milioni 27 ambazo klabu hiyo ilimnunua (Liverpool Echo)
Mshambulizi wa
Liverpool Danny Ings, 25, amasema itakuwa uamuzu wa upuuzi kuondoka Anfield mwisho wa msimu. (Sunday Express)
Jack Butland |
Liverpool wana uhakika wa kufanikisha rekodi ya pauni milioni 40 kwa kipa wa England na Stoke City wa miaka 24 Jack Butland. (Sunday Mirror)
Neymar |
Manchester United wana mpango wa kumtafuta beki wa Juventus Mbrazil Alex Sandro, 27, msimu ya joto. (Sunday People)
Paris St-Germain wako wazi katika kumuuza mshambulizi Neymar, 26, kwa klabu yake ya zamani Barcelona au kwa washindani wao Real Madrid. (Sky Sports)
Real Madrid watamwinda kipa ya Hajduk Split Karlo Letica 21, ikiwa hawataweza kumpata kipa wa Manchester United David De Gea,27, au kipa wa Chelsea Mblegiji. Thibaut Courtois (Marca)
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike ffacebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
Post a Comment