WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe |
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema atawasilisha kwa Waziri Mkuu majina ya maofisa habari wazembe, ili watumbuliwe.
Alisema hayo kufuatia uzembe unaofanywa na baadhi yao huku wakibweteka kukaa maofisini bila kufanya kazi.
Alisema maofisa habari wasiojituma ni sawa na kuwa na maofisa habari hewa, ambao wanakula mishahara wasioifanyia kazi, jambo ambalo hakubaliani nalo.
Dk. Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa kazi wa siku tano wa maofisa habari, mawasiliano na uhusiano serikalini, unaofanyika jijini hapa, aliwataka kubadilika na kutekeleza malengo waliojiwekea.
"Kweli naangalia tovuti za halmashauri zipo tisa tu zinazofanya vizuri, zingine wahusika wamelala; na mikoa 18 tu inafanya vizuri kuhabarisha, sasa hawa wengine wajitathmini vinginevyo nitapeleka majina yao kwa Waziri Mkuu, ili watumbuliwe, tutoe ajira kwa wengine," alisema.
Aliwataka wafanye kazi ya kuhabarisha wananchi kazi zinazofanywa na serikali, ili wasitumbuliwe, Alisema hata wizara husika pia wapo wazembe nao atapeleka taarifa ngazi ya juu ili wachukuliwe hatua, lengo kazi nzuri zinazofanywa na serikali zitambulike kwa wananchi na kuziba mianya kwa wapotoshaji wa taarifa za serikali.
Dk. Mwakyembe aliwataka maofisa habari hao kujituma na kutoa taarifa za kazi zinazofanyika kila siku kwenye mitandao ya kijamii na endapo watazuiwa na mtu yeyote, wawafichue hata kwa siri ili wizara ishughulike na muhusika.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Alvaro Rodriguez, aliwataka maofisa habari hao kubadilika na kuleta tija kwa taifa baada ya mkutano huo kuisha.
Alisema dunia sasa imeunganishwa kwa teknolojia, hivyo ni vema jamii ikapata taarifa zilizo sahihi kwa wakati.
Aidha, alisema serikali pia inahitaji kusikiliza jamii na sauti za wananchi, ili kupiga hatua katika kufikia Tanzania ya Viwanda.
“Sisi kama wadau tunahitaji kusikia zaidi habari za wananchi wa vijijini, ili tuone jinsi wanavyobadilika katika hali walizonazo,” alisema.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Post a Comment