MANENO YA CONTE BAADA YA KUPOKEA KICHAPO CHA 3-0 KUTOKA KWA BARCELONA

Lionel Messi alifunga bao lake la 100 katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na kusaidia kuwalaza Chelsea 3-0 uwanjani Nou Camp

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema alihisi kwamba kichapo cha 3-0 ambacho klabu yake ilipokezwa katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano "hakikuwa cha haki".

Lionel Messi alifunga mabao mawili naye Ousmane Dembele akafunga moja - bao lake la kwanza akichezea Barca - na kuwasaidia miamba hao wa Uhispania kuondoka na ushindi wa jumla wa 4-1.

Mechi ya kwanza uwanjani Old Trafford ilikuwa imemalizika 1-1.

Matokeo hayo yaliwaondoa Chelsea kutoka kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu na msimu ujao wanakabiliwa na kibarua cha kufuzu kutokana na ushindani mkali kwenye nafasi nne za kwanza Ligi ya Premia.

"Hatuna majuto," alisema Conte.

"Ukiitazama mechi hiyo, utaona kwamba matokeo hayo hayakuwa ya haki."

Conte alikiri kwamba Messi - aliyefunga pia bao la Barca mechi ya kwanza Stamford Bridge - ndiye aliyekuwa mwamuzi wa nani mbabe kati ya timu hizo mbili.

Bao la pili la mshambuliaji huyo wa Argentina uwanjani Nou Camp lilifikisha 100, idadi ya mabao ambayo ameyafunga Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Lionel Messi akipongezwa na meneja wa Chelsea Antonio Conte baada ya mechi Jumatano


Mpinzani wake mkuu kutoka Real Madrid Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi akiwa na mabao 117.

Hata hivyo, Messi amefikisha idadi hiyo akiwa amecheza mechi 14 chini ya alizocheza Ronaldo ndipo afikishe mabao hayo.

"Tunazungumzia mchezaji bora zaidi duniani," alisema Conte.

"Huwa anafunga mabao 60 kila msimu - ni mchezaji mzuri ajabu. Barcelona walikuwa na ufasaha sana wakishambulia."

Klabu nane zilizofuzu..
Klabu zilizofika robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu ni: Barcelona, Bayern Munich, Juventus, Liverpool, Manchester City, Real Madrid, Roma na Sevilla.
Droo itafanyika Nyon, Uswizi saa 11:00 GMT Ijumaa


Chelsea waliongoza kwa dakika 13 mechi ya kwanza na waligonga mwamba na mlingoti wa lango mara nne katika mechi zote mbili.

N'Golo Kante na Marcos Alonso wote walikaribia kufunga uwanjani Nou Camp, naye Antonio Rudiger alipiga mpira wa kichwa ambao uligonga mwamba wa goli dakika za mwisho.

Blues walinyimwa ombi lao la kutaka penalti Alonso alipoanguka eneo la hatari baada ya kukabiliwa na Gerard Pique.

"Hatukustahili kushindwa 3-0," alisema Conte.

"Tulikosa bahati kiasi.

"Tafikiri tulitengeneza naafsi nyingi lakini hatukuzitumia.
Wachezaji wa Chelsea waliotamauka wakiondoka uwanjani baada ya kushindwa Nou Camp

"NI lazima nijivunie sana wachezaji wangu - walijitolea kabisa na ni lazima tuendelee hivi, nia hii ya kupambana na kupigana vita pamoja uwanjani." 


Courtois hatarajia kombora la Messi

Mlindalango wa Chelsea Thibaut Courtois aliambia BT Sport kwamba anaamini makosa ya wachezaji binafsi yaliigharimu timu hiyo.

"Sifikiri kwamba tulifaa kuondolewa, lakini makosa ya wachezaji binafsi  ushindi mechi zote mbili.

"Bao la kwanza ... Sikutarajia Lionel Messi angetoa kombora kutokana na pahali ambapo alikuwa na nilichelewa kufunga mwanya kati ya miguu yangu. Hilo lilikuwa kosa langu.
Antonio Conte atakutana na Wachezaji wa Chelsea waliotamauka wakiondoka uwanjani baada ya kushindwa Nou Camp Jumapili kupigania nafasi ya kufuzu kwa nusufainali katika Kombe la FA

"Pahali dhaifu zaidi huwa ni katikati ya miguu ya golikipa. Inaudhi. Siwezi kujificha ndani (ya lango), ni lazima niwe kama mwanamume na kutokea."

Winga wa Chelsea Marcos Alonso aliambia BT Sport kwamba walifahamu kwamba Barca wana wachezaji wazuri sana.

"Na hatuwezi kuwapa nafasi, hata mita moja, kwa sababu wanaweza kuunda nafasi na kufunga."
Lionel Messi akisherehekea baada ya kuwafunga Chelsea

Amesema sasa ni lazima warudi kujiboresha zaidi, kufanya mazoezi na "kujiboresha".

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post