IJUE REKODI YA MADAKTARI WANAOMTIBU TUNDU LISSU

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.


HUU ndio ukweli! Madaktari wawili waliobobea wanaomtibu Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu, Profesa Stefaan Nijs na Profesa Willem-Jan Mertsemakers wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg, Ubelgiji ni wataalamu waliobobea kwa upasuaji barani Ulaya, UWAZI limegundua.

Kwa mujibu wa mtandao wa hospitali hiyo ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg Ubelgiji,madaktari hao wametajwa kuwa ni wataalamu wa ubasuaji wa hali ya juu wanaotegemewa katika Bara la Ulaya.Maprofesa hao wamebainishwa kuwa ndio waliofanya kazi kubwa kuokoa maisha ya majeruhi wa bomu lililolipuliwa na magaidi Machi mwaka jana nchini Ubelgiji.

“Profesa Stefaan Nijs ambaye ni mkuu wa idara ya mafunzo ya udaktari chuoni hapo ndiye aliyeongoza kikosi cha madaktari wengine akiwemo Profesa Willem- Jan Mertsemakers kutibu na kuwafanyia upasuaji waliojeruhiwa na bomu, yeye na timu yake ndio waliowafanyia upasuaji wa hali ya juu waathirika wa mlipuko wa bomu na kuokoa maisha ya majeruhi wengi, ”lilisema gazeti Telegraph nchini humo.

Imeelezwa kuwa madaktari hao ni maarufu siyo tu Ubelgiji, bali pia nchi mbalimbali za Ulaya na wameshapewa tuzo mbalimbali kutokana na kuokoa maisha ya watu sehemu mbalimbali duniani.

Habari kutoka Hospitali ya Leuven na kuthibitishwa na Lissu ambaye pia Mwenyekiti wa Chama Cha Wanasheria Tanzania (TLC),zinasema madaktari hao ndio waliogundua kuwa goti la mwanasiasa huyo lina shida kubwa na linahitaji upasuaji la sivyo hata kama angepona kungewezekana kuvunjika tena siku za usoni.


Profesa Stefaan Nijs.

Lissu tayari amefanyiwa upasuaji kama alivyoshauriwa na madaktari hao na alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema operesheni hiyo iliyochukua saa mbili, ilifanywa na timu ya madaktari bingwa chini ya uongozi wa Profesa Willem-Jan Mertsemakers.“Operesheni ilienda vizuri na kwa sasa naendelea na dawa na mapumziko hospitalini kwa muda wa angalau wiki tatu zinazokuja, ” alisemaLissu katika taarifa yake.

Akaongeza: “Wameniwekea chuma cha kuimarisha mfupa wote wa paja la kulia. Pia wamechukua vipimo ili kuangalia kama hakuna tatizo la bacteria kabla hawajafunga kabisa sehemu ya kwenye goti ambayo haijaunga hadi sasa.

”Mke wake, Alicia Lissu alisema anamshukuru Mungu kwamba upasuaji huo umekwenda vyema.Wakati Lissu akisema hayo huko Ubelgiji, kaka yake,Wakili Alute Mughwai ambaye ndiye msemaji wa familia yao,alisema wameelezwa kuwa baada ya siku 10, madaktari watatoa taarifa juu ya maendeleo ya afya yake na mazoezi ya viungo ambayo alikuwa anaendelea nayo.

Alipoulizwa na gazeti hili atarudi lini ndugu yake alikuwa na haya ya kusema:“Kutokana na maelekezo ya madaktari kwa sasa, hatuwezi kusema Lissu atarudi lini nchini, kwani upasuaji (aliofanyiwa wiki iliyopita) umesababisha alazwe tena hospitali,” alisema.

Mughwai aliwashukuru Watanzania wanaoishi Ubelgiji kwa mchango mkubwa wanaotoa katika matibabu ya Lissu, kama ilivyokuwa kwa Watanzania wanaoishi Nairobi, Kenya. Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017akiwa nyumbani kwake mkoani Dodoma alipokuwa anahudhuria vikao vya bunge, baada ya shambulizi alipelekwa Nairobi Kenya kwa matibabu na baada ya miezi mitatu alisafirishwa kupelekwa nchini Ubelgiji kwa hatua nyingine ya matibabu ambako ndipo alipo.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post