Shirikisho la Soka Barani Africa (CAF), limefanya mabadiliko ya ratiba katika baadhi ya michezo ikiwemo wa Simba dhidi ya Al Masry SC katika Kombe la Shirikisho.
Awali mechi hiyo ilipangwa kuchezwa tarehe 6 huku Simba wakianzia nyumbani, lakini sasa utafanyika March 9 2018 baada ya tarehe ya mwanzo kuingiliana na mechi ya Yanga.
Ratiba ya awali ilionesha Yanga watakuwa wenyeji wa Township Rollers FC kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, ambayo ilitakiwa kupigwa March 6 2018.
Baada ya mabadiliko hayo, sasa Simba wataanzia nyumbani kama ilivyokuwa mwanzo na mchezo wa marudiano ratiba inaonesha mchezo utapigwa March 16 2018.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Post a Comment