SIMBA YADHIIRISHA UNYAMA WAKE MBELE YA GENDARMARIE



SIMBA SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Gendarmarie Tnare jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo uliotokana na mabao ya wazawa, kiungo Said Hamisi Ndemla, Nahodha na mshambuliaji John Raphael Bocco na mshasmbulaiji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi – wazi Simba itakuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo Djibouti.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Alier Michael James aliyesaidiwa na Abdallah Suleiman Gassim na Gasim Madir Dehiya washika vibendera, Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa mabao 3-0.

Kiungo Said Ndemla alizindua shangwe za mabao Simba SC dakika ya kwanza tu baada ya kufunga kwa shuti la kiufundi la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20, kufuatia Bocco kuchezewa rafu.
Bocco akaifungia Simba SC bao la tatu dakika ya 32 kwa kichwa, akitumia mwanya wa kipa wa GendarmerieTnare kuanguka katika harakati za kuokoa.

Mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Bocco akafunga bao la tatu dakika ya 45 kwa kichwa tena akimalizia pasi nzuri ya mshambuliaji mwenza, Mganda Emmanuale Okwi.

Kipindi cha pili, Simba inayofundishwa na kocha Mfaransa, Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mtunisia, Mohamed Aymen Hbibi, Mrundi, Masoud Juma na mzalendo, Muharami Mohamed ‘Shilton’ kocha wa makipa haikuwa na makali iliyoanza nayo.

Na dakika ya 50 Gendarmerie wakapoteza nafasi nzuri ya kupata bao la ugenini baada ya mkwaju wa penalti uliopigwa na Moustapha Moussa kufuati Abdorahim Mohamed kuangushwa kwenye boksi na kiungo Mghana, James Kotei kuokolewa na kipa namba moja Tanzania, Aishi Manula.

Na baada ya mchezo kupooza kwa takriban nusu saa, Mganda Okwi aliyepoteza nafasi nyingi za kufunga leo, akasahihisha makosa yake kwa kufunga bao la nne dakika ya 90 baada ya kuanzishiwa pasi ya pigo la adhabu ndogo na beki anayemudu kucheza kama kiungo pia, Erasto Nyoni.

Mapema kabla ya kuanza kwa mchezo huo, mgeni rasmi, Rais wa awamu wa pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi 'aliwatia baraka' wachezaji wa Simba kwa kuwasabahi uwanjani na kuwatakia kila la heri.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Yussuph Mlipili, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Muzamil Yassin dk72, Said Ndemla/Mwinyi Kazimoto dk75, James Kotei, John Bocco na Emmanuel Okwi.

Gendarmerie Tnale; Bilal Ahmed, Houmaye Ali, Samatar Hassan, Moustapha Moussa/Yabeh Idriss dk58, Mohamed Idris, Moussa Youssouf, Abdorahim Mohamed/Kader Aden dk80, Mohamed Mogbel, Ahmed Aden, Souhaib Ismil/Osman Mohamed dk55 na Andre Rene.
Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post