Nyota wa FC. Barcelona, Lionel Messi, ameweza kuvunja rekodi ya kutofunga goli lolote dhidi ya Chelsea pindi timu hizo zinapokutana akiwa na timu yake.
Imemchukua mchezaji kutumia dakika 730 na mechi 9 kufunga bao lake la kwanza katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya (UEFA), ikiwa ni dakika ya 75 ya mchezo.
Messi ambaye amekuwa yuko katika kikosi kimoja na Andres Iniesta tangu aanze kuichezea Barcelona mpaka sasa, alikuwa hajawahi kuzigusa nyavu za Chelsea.
Iniesta ndiye alimsaidia Messi kufunga bao hilo kwa pasi safi ikitokea upande wa kushoto mwa uwanja wa Stamford Bridge, na bila jinamizi akaipasia golini moja kwa moja.
Bao lake la kusawazisha limekuwa muhimu kwa Barcelona ambayo imekuwa na faida ya goli moja la ugenini, kabla timu hizo hazijakutana tena katika mchezo wa marudiano.
Mechi ya marudiano itachezwa kwenye Uwanja wa Camp Nou, Jumatano ya March 14 2018.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Post a Comment