TRUMP ATISHIA KUSITISHA MSAADA NCHINI PALESTINA


Rais wa Marekani Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kukata msaada wa kifedha kwa serikali ya Palestina, kwa maelezo kwamba Marekani inawalipa mamia ya mamilioni ya dola za kimarekani kwa mwaka na hakuna chochote inachoambulia , hakuna cha shukrani ama heshima kutoka kwa taifa hilo.

Katika utamaduni aliojijengea rais wa Marekani ,Donald Trump wa utumizi wa mtandao wa kijamii wa twitter kama sehemu yake ya kutolea matamko , rais amesema kwamba Wapalestina hawana mpango wowote wa kuwa na mazungumzo ya maridhiano na amani na Israel na kuhoji uhalali wa Marekani kuendelea kujitoa kwa kiasi hicho.

Mwezi uliopita rais wa Palestina Mahmoud Abbas alitoa tamko la taifa lake kutokuwa tayari kupokea mpango wowote wa amani kutoka Marekani, baada ya mji wa Washington kuitambua Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli.

CHANZO BBC

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post