ACT WAZALENDO NA CHADEMA WAPOTEZA VIONGOZI 18; WAHAMA VYAMA VYAO NA KUJIUNGA NA CCM


 ACT VS CCM
TUNAKUOMBA KUFOLLOW NA KUSUBSCRIBE KATIKA WEB YETU NA MITANDAO YA KIJAMII ILI KUTUMIWA UPDATES WAKATI WOWOTE.
Viongozi 18 wa chama cha ACT-Wazalendo kutoka mikoa mbalimbali nchini wamejivua nyadhifa zao na kujiunga na CCM.

Viongozi hao wamepokelewa leo Januari 17, 2018 mjini Moshi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ambaye hivi karibuni alihamia chama tawala. Mghwira amewahi kuwa mwenyekiti wa ACT.

Miongoni mwa wanachama hao, wapo waliokuwa wajumbe wa kamati kuu, wenyeviti wa mikoa na makatibu wa ACT.

Pia, viongozi 18 wa Chadema ngazi za kata na vijiji kutoka Wilaya ya Siha nao wamejiunga na CCM.

Akizungumza baada ya kuwakaribisha, Polepole amesema katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano, CCM kimeongeza wanachama zaidi ya milioni mbili.

"Tukisimamia haki na heshima kwa watu wote CCM kitatawala milele nchi hii. Kwa sababu misingi ya chama hiki ni utu. Sasa tunahitaji watu ambao wanachukizwa na rushwa, ubadhirifu na ubinafsi,” amesema Polepole.

Kwa upande wake Mghwira amesema siasa bado ina changamoto kubwa na kuwataka wanasiasa kufanya siasa za kuwaunganisha watu pamoja, si kujenga uadui.

"Nchi haiwezi kujengwa kwa maneno ya kashfa…,ili tupige hatua kimaendeleo inatakiwa idadi ya vyama vya siasa ipungue kwa sababu utitiri wa chama ni mkubwa ikilinganishwa na ukubwa wa nchi yete,” amesema Mghwira.

Aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya ACT, Kansa Mbaruku amesema wamechukua maamuzi hayo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo ya viongozi waandamizi wa chama hicho kuhama, akiwemo Mghwira .

Baadhi ya viongozi hao ni Eva Kaka (mjumbe Kamati Kuu), mwenyekiti wa Mkoa wa Dodoma Anganile Massawe, Athuman Balozi (mwenyekiti mkoa wa Tabora), Hamad Nkya (mwenyekiti mkoa wa Kilimanjaro), Godwin Kayoka (katibu wa mkoa Tabora) na Juma Hamisi (mwenyekiti wazee mkoa wa Singida).EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.

 BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post