Zikiwa zimesalia siku 3 pekee dirisha dogo la Usajili Ligi Kuu Tanzania bara kufungwa mpaka Sasa klabu ya Simba bado haijatangaza kukamilisha Usajili Wa mchezaji yeyota licha ya tetesi ambazo zimekua zikipita kunako mitandao mbalimbali na vyombo mbalimbali vya habari.
METHOD MWANJALI
Asubuhi hi tuziangazie baadhi ya tetesi ambazo zimeshika hatamu kunako klabu hiyo ambapo katika Hilo tutaanza na taarifa iliyotoka kwa siku ya jana ambapo taarifa hiyo inaeleza kuwa klabu hiyo imempatia mkono Wa kwaheri Nahodha wake Na mlinzi Wa kimataifa kutoka Zimbabwe, Method Mwanjali.
Sababu zinazotajwa no pamoja Na Majeruhi ya Mara kwa Mara huku baadhi ya mashabiki pia wakidai umri pia unachangia.
JONAS SAKUHAWA NA LAUDIT MAVUGO.
Katika hatua nyingine klabu ya Simba i
meonekana kuridhishwa Na uwezo aliouonyesha mshambuliaji kutoka Zambia,Jonas Sakuhawa katika michezo Wa kirafiki Dhidi ya KMC Na hivyo kufikilia kuachana Na Mrundi, Laudit Mavugo.
Sakuhawa mwenye miaka 34, anajiunga Na Simba katika dirisha dogo huku akiwa Na historia ya kuvitumikia vilabu vikubwa barani Afrika ikiwemo klabu za TP Mazembe na Zesco United.
Sakuhawa mwenye miaka 34, anajiunga Na Simba katika dirisha dogo huku akiwa Na historia ya kuvitumikia vilabu vikubwa barani Afrika ikiwemo klabu za TP Mazembe na Zesco United.
KUHUSU NAHIMANA SHASSIR(RAYON SPORTS)
Klabu ya Simba imejiondoa katika kinyang’anyiro cha kumsaka straika wa Rayon sports, Nahimana Shassir baada ya Kuonekana kushuka Kiwango.
Shassir ambae ni raia wa Burundi alipendekezwa na kocha msaidizi wa klabu hiyo ya wekundu wa msimbazi, Masoud Djuma, lakini kutokana na kutokuwa na kiwa cha kiridhisha kwa wakati huu kocha huyo ameamua kuachana naye.
Djuma alisema: “Nilipendekeza asajiliwe lakini mpaka sasa tumesitisha dili hilo kwa sababu ameshuka kiwango, nimemuangalia kwenye michuano ya Chalenji nimeona hajaisaidia chochote timu yake, hivyo hatutamsajili tena.
“Hatuwezi kumsajili mchezaji wakati uwezo wake ni mdogo kuliko wale waliopo ndani ya kikosi chetu cha Sasa”.
Mzamiru Yassini Na Jjuuko Morshidi.
Aidha uongozi was klabu hiyo umesema kuwa tayari ufikia muafaka na Nyota wake Wa will ambao walikuwa wakihusishwa na kuondoka kunako klabu hiyo huku ikielezwa kuwa wamekubali kusaini mkataba mpya.
Nyota hao no Mganda, Jjuuko Morshidi na Mtanzania Mzamiru Yassini ambao happy awalo walitajwa kuondoka klabuni humo huku ikielezwa kuwa wangeelekea kunako mitaa ya Twiga na Jangwani( Yanga).
Asante Kwasi Atatua Simba?
Majuma kadhaa yaliyopita zilizagaa taarifa zinazomuhusisha beki kisiki Wa klabu ya Lipuli Fc , Asante Kwasi kujiunga na Simba ambapo ilielezwa kuwa beki huyo tayari ameranya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo na atajiunga mnamo dirisha dogo hili.
Kwasi ambae mpaka Sasa ameshafunga magoli 5 huku ikielezwa kuwa ndie beki mwenye idadi kubwa ya magoli.
Kwa taarifa za Chini ya Kapeti mpendwa msomaji Wa vyankende.com ni kuwa beki huyo ananafasi kubwa ya kusajiliwa ili kuziba nafasi ya aliyekuwa Nahodha Wa klabu hiyo Method Mwanjali.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Post a Comment