SABABU YA LULU KUKOSA MSAMAHA WA RAIS DEC, 09


Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Juma Malewa amesema katika msamaha uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli siku ya uhuru Desemba 9, 2017 haukumuhusu msaani wa filamu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu.

Jenerali Malewa amefafanua kuwa mchakato wa kuanza kuangalia wafungwa wakupunguziwa vifungo na kusamehewa haukumuhusisha Elizabeth Michael kutokana na yeye kuingia gerezani wakati tayari mchakato wa kuangalia wafungwa wa kusamehewa na kupunguziwa vifungo ulikuwa umeshaisha

"Msamaha huu haukumuhusu yeye kwa sababu aliingia magereza wakati tayari zoezi hili lilikuwa limekamilika, kwahiyo labda misamaha ijayo kama itakuwepo lakini katika hii haikumuhusu",amesema Kamishna Malewa.

Kamishna Malewa pia ameeleza kuwa vipo vigezo vingi vinavyoweza kumfanya mfungwa asamehewe ama kupunguziwa kifungo kutokana na kosa na muda wa kifungo chake na kwamba misamaha inatofautiana kutokana na kosa kama endapo mfungwa atafata taratibu na kuonekana amerekebishika anaweza kupata msamaha na mengine mengi.

Desemba 9 mwaka huu siku ya uhuru kwa mujibu ya ibara ya 45 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais John Pombe Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Nguza Viking (Babu Seya ) na Johnson Nguza (Papii Kocha ) waliohukumiwa kifungo cha maisha jela na wengine kupunguziwa vifungo vyao.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post