TETESI ZA SOKA LA ULAYA 25.10.2017



Mesut Ozil

Michael Appleton anatarajiwa kuacha wadhifa wa kaimu meneja wakati Leicester wanakaribia kumteua aliyekuwa maneja wa Southmpton Claude Puel. (Daily Telegraph)

Manchester United haijachukua hatua ya kumpata mshambuliaji wa Arsenal Mesut Ozil, lakini ni kati ya vilabu vitatu ambavyo mchezaji huyo wa miaka 29 raia wa Ujerumani angepenada kuhamia akitoka Arsenal. (Manchester Evening News)

Rais wa Real Madrid Florentino Perez anasema hajamfikiria Harry Kane licha ya uvumi kuwa klabu hiyo ilikuwa inamwinda mshambuliaji huyo wa Tottenham na England. (Daily Mirror)Harry Kane (kulia)

Mshambuliaji raia wa Senegal Diafra Sakho, 27, anasema anataka kuondoka West Ham. (Claude Atcheba

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amekana madai kuwa mchezaji wa safu ya kati Charly Musonda, 21, anaruhusiwa kukihama klabu hiyo mwezi Januari kwa mkopo. (Daily Express)

Ajenti wa mchezaji wa kiungo cha kati wa Southampton Sofiane Boufal, 24, anadai vilabu vya Italia vya Fiorentina na Inter Milan vilitaka kumsaini. (SFR Sport via Talksport)Thomas Tuchel

Aliyekuwa meneja wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel, 44, hajakataa ikiwa atakubali kuwa meneja wa Everton ikiwa ataombwa kufanya hivyo. (Sky Sports)

Meneja wa West Ham amekataa kulaumu kusainiwa wachezaji wapya baada ya kushindwa nyumbani na Brighton Ijumaa iliyopita. (Evening Standard)

Marekani inatathmini miji ambayo inaweza kuomba kuandaa kombe la dunia mwaka 2016. (Washington Post)Danny Ings

Crystal Palace wana nia ya kumsaini Danny Ings, 25, kutoka Liverpool kwa mkopo mwezi Januari lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa vilabu vingine vitatu. (News Shopper)

Manchester United na Arsenal wanamfuatilia Marco Reus huko Borussia Dortund. (Sky Sports Germany, via Daily Mirror)

Rais wa Real Madrid Florentino Perez anasema kuwa itagharimu pauni milioni 223 kumnunua mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 24. (Calciomercato)

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI








0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post