TETESI ZA SOKA ASUBUHI YA LEO



Image result for SOCCER UPDATES
Huenda Barcelona ikarejea tena Liverpool kufanya mazungumzo juu ya kumsajili nyota , Phillipe Coutinho huku taarifa zikieleza kwamba, Lionel Messi huenda akaachwa aondoke mwezi Januari
Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane amefungua milango kwa timu yoyote inayohitaji huduma yake.
Victor Lindelof, amekanusha tetesi zinazosema aliwahi kukutana uso kwa uso na kocha, Jose Mourinho.
Nyota wa Borussia Dortmund, Marco Reus anafikiria kuihama klabu hiyo siku za usoni.
Theo Walcott anahusishwa kujiunga na Everton.
Virgil van Dijk anaamini huenda akaachana na Southampton mwezi Januari.
Ivan Perisic, huenda asijiunge tena na Manchester United baada ya kiwango cha Antony Martial kuimarika zaidi.
Pep Guardola anajua jina la kocha mpya wa Bayern Munich, kwa mujibu wa Rais wa klabu hiyo ya Ujerumani.
Guardiola ambaye alifanya kazi kwa mafanikio kwa miaka mitatu katika dimba la Allianz Arena kabla ya kuhamia Manchester City mwaka jana, jana Jumanne alikula chakula cha jioni na Rais wa Bayern Munich Uli Hoeness
"Guardiola aliniahidi kwamba kila mwaka atakuwa anakuja Oktoberfest , ulikuwa mkutano baina ya marafiki wawili lakini pia tulizungumzia mambo ya kazi . Nilimuambia jina la kocha ambaye tutamuajiri katika siku chache zijazo na aliridhika."
Thomas Tuchel, Louis van Gaal na Luis Enrique wote wamehusishwa na kazi hiyo tangu wiki iliyopita ambapo kuna taarifa zinasema kwamba Enrique anatarajiwa kukutana na uongozi wa Bayern Munich jana Jumatano.

Mwekezaji namba mbili mkubwa wa Arsenal Alisher Usmanov amesema hafanyi mazungumzo yoyote na mwenye hisa nyingi katika klabu hiyo Stan Kroenke kuhusu kuuza hisa zake katika klabu hiyo.

Imeripotiwa kwamba Kroenke ambaye anamiliki 67% za hisa ametoa ofa ya kununua ofa za Usmanov ambazo zinafika asilimia 30.

Hata hivyo Usmanov, 64, amesema kwamba maslahi yake Arsenal ni 'ya 'muda mrefu'.

"Naziona hisa zangu za asilimia 30 ni kitu muhimu sana katika kulinda maslahi ya mashabiki katika klabu."

Licha ya kuwa mwanahisa, Usmanov hayupo kwenye bodi au wata wanaofanya maamuzi ndani ya klabu na hivi karibuni alimkosoa Kroenke kuhusu mwenendo mbaya wa klabu.

Usmanov mnamo mwezi Mei alitoa ya Pauni Bilioni 1 kuimiliki klabu lakini ilikataliwa na Kroenke.

"Maslahi yangu kwa Arsenal tangu awali yalikuwa ni ya muda mrefu na mipango yangu siku zote ilikuwa ni kununua hisa zaidi kama zikiwekwa sokoni."

Gerard Pique amesisitiza kwamba hatoacha kucheza timu ya taifa ya Hispania licha ya kuzomewa na mashabiki wa taifa hilo baada ya kutokea kwa machafuko jijini Catalunya.

Beki huyo wa Barcelona amesisitiza kwamba 'haiwezekani' kutilia shaka kujitoa kwake kwa moyo wote katika 'Familia' ambayo amekuwa akiitumikia tangu alipokuwa mdogo.

Akiongea na vyombo vya habari kuelekea kwenye mechi ya kufuzu kucheza kombe la Dunia dhidi ya Albania, Pique amesema," Tangu mwanzo wa hali hii kuwa na mashabiki ambao awali walikuwa wakikushangilia halafu sasa hivi wana kupigia miluzi na kukutukana, imekuwa ngumu sana kwangu."

"Lakini haiwezekani hata kidogo kutilia shaka kujitoa kwangu katika taifa hili tangu nikiwa na umri wa miaka 15 . Naiona hii kama Familia na ndio moja ya sababu kwanini naendelea kuitumikia."

Baada ya vipimo kufanyika kwa Dani Carvajal, amegundulika na maambukizi ya virusi vinavyoshambulia ukuta uliozunguka moyo ( viral pericardium infection ).

Taarifa kutoka Real Madrid inasomeka hivi," Baada ya vipimo kufanyika kwa Dani Carvajal, amegundulika na maambukizi ya virusi vinavyoshambulia ukuta uliozunguka moyo "

Lakini Real Madrid wamegoma kubonyeza kitufe cha hofu ( Panic Button ) na hawatosajili beki mwingine majira ya baridi . Los Blancos wanataka Nacho awe mbadala wa Carvajal pindi Marcelo na Theo Hernandez watakapopona, lakini kwa muda huu beki chipukizi wa Morocco Achraf Hakimi hatokuwa na presha yoyote ya kuziba pengo la Carvajal.

Vilabu vya Ligi kuu ya Uingereza vimekubali kufanya mazungumzo zaidi kuhusu mapendekezo mapya ya kubadilisha jinsi ya kupokea fedha za mikataba ya matangazo nje ya nchi.

Vilabu vimekutana mapema leo kuzungumzia swala hilo na bila kupingwa imekubaliwa kuharisha kikao ili kuruhusu mazungumzo zaidi.

Vilabu havijakataa mapendekezo yoyote kuhusu mgawanyiko wa mapato wa matangazo ya kimataifa lakini wanachokitaka ni kuwepo na mazungumzo zaidi.

Jana Jumanne Sky Sports waliripoti kwamba vilabu vilipendekeza ile asilimia 35 ya mapato ya matangazo ya television nje ya nchi yagawanye kwa mujibu wa nafasi ya klabu inapomaliza katika msimamo wa ligi , na zile asilimia 65 zinazobaki zigawanywe sawa kwa sawa kwa vilabu vyote.

Asilimia 100 ya mapato kutoka nje ya nchi kwa sasa yanagawanywa sawa kwa sawa katika mfumo wa sasa na kila klabu inapokea takribani pauni milioni 39 kutoka kwenye mapato hayo ya nje ya nchi.

Manchester City, Manchester United, Tottenham, Chelsea, Arsenal na Liverpool wameripotiwa kutaka mabadiliko ya mfumo wa sasa wa mgawanyo sawa wa mapato kutoka nje ya nchi .

Baadhi ya vilabu ambavyo vinaamini kwamba vinaingiza mapato makubwa sana wanatakiwa kupokea kiasi fulani kikubwa cha mapato ya nje ya nchi kutokana na uuzaji wao wa kimataifa na uwekezaji.

Vilabu tisa kwa sasa vinakubaliana na mpango mpya wa mgawanyo , ambapo vilabu 14 vinatakiwa kukubali mpango mpya kabla ya kupitishwa.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI








0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post