SIMBA MANUSULA WAPOTEZE MCHEZO WAO DHIDI YA MTIBWA SUKARI



MPIRA UMEKWISHAAAA
GOOOOOOOOOOOOOO Dk 90+3 Okwi anaisawazishia Okwi kwa mpira wa adhabu, anaachia mkwaju mkali unaomshinda unaomshinda kipa Tinocco
SUB anatoka Kihimbwa, anaingia Henry Joseph upande wa Mtibwa


OKWIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Inapigwa, inakuwa faulo nyingine nje kidogo ya eneo la penalti, wachezaji wa Simba wanalalamika kuwa ni penati

Dakika ya 93: Simba wanapata faulo karibu na eneo la 18 la Mtibwa.

Dakika ya 89: Mambo bado ni magumu kwa Simba.

Dakika ya 86: Mtibwa wanafanya shambulizi kali, Manula anaokoa inakuwa kona, inapigwa inaokolewa tena na kipa huo.

Dakika ya 83: Simba wanapanda, wengi wao wanapanda mbele kutafuta bao la kusawazisha, Mtibwa wanapiga pasi ndefu.

Dakika ya 82: Mtibwa wanafanya shambulizi kali, lakini beki Ally Shomari anafanya kazi nzuri ya kuokoa.

Dakika ya 78: Erasto Nyoni anatengeneza nafasi za kupiga krosi lakini bado mambo ni magumu.

Dakika ya 74: Presha imekuwa kubwa kwa Simba kulishambulia lango la Mtibwa Sugar.

Dakika ya 73: Simba wanamiliki mpira muda mwingi, sasa wanatengeneza pasi na nafasi nyingi.

Dakika ya 64: Simba wanafaanya mabadiliko, anatoka Kichuya, anaingia Said Ndemla

Dakika ya 59: Simba wanafika langoni mwa Mtibwa lakini wanashindwa kutumia nafasi.

Dakika ya 57: Mshambuliaji wa Mtibwa anaumia, anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Kelvin Kongwe.

Dakika ya 52: Mbonde anashindwa kuendelea, anatoka, nafasi yake inachukuliwa na Juuko Murshid.

Dk 51, basi nzuri sana ya Mohamed Issa lakini Stamili Mbonde anaikosa kidogo tu na kuanguka mwenyewe. Yuko chini anatibiwa
SUB Dk 49 Mbode anatoka kwa upande wa Simba na nafasi yake inachukuliwa na Mganda, Juuko Murshid

Dk 45 Kipindi kimeanza na inaonekaan Simba wanataka kusawazisha lakini Mtibwa wanataka kuongeza bao la pili

MAPUMZIKO

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Niyonzima anaachia mkwaju wa faulo lakini unakuwa nyanya kabisa kwa kipa
Dk 42 Nyoni anacheza kona nyingine nzuri kabisa hapa, lakini safari Mtibwa Sugar wanaokoa vizuri kabisa
Dk 41, Kotei anaachia mkwaju inakuwa kona, inachongwa wanaokoa tena inakuwa kona
Dk 38, Simba wanaingia vizuri lakini shuti kali la Okwi linapaa juuu
GOOOOOOOOOO Dk 36, kona safi, mabeki wa Simba wakiwa wmazubaa, Mbonde anaruka na kufunga kwa kichwa

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 35: Mtibwa wanapata kona mbili mfululizo, Aishi Manula anafanya kazi njzuri kuokoa.

Dakika ya 24: Viungo wa Simba wanaonyesha kuelewana muda mwingi kutokaan na kupigiana pasi.

Dakika ya 24: Viungo wa Simba wanaonyesha kuelewana muda mwingi kutokaan na kupigiana pasi.

Dakika ya 20: Simba wanapiga shuti la mbali lakini mpira unatoka.

Dakika ya 17: Simba wanafanaya mabadiliko, anaingia Juma Liuzio, ametoka Bocco ambaye aliumia mguu.

Dakika ya 13: John Bocco anaumia, amekaa chini, anaonyesha ishara hawezi kuendelea na mchezo, anatolewa nje.

Dakika ya 9: Mtibwa wanalisogelea lango la Simba lakini mpira unaokolewa.

Dakika ya 8: Mkude anapata nafasi ya kupiga pasi nzuri anashangiliwa sana na mashabiki wa timu yake.

Dakika ya 5: Simba wanapata kona, inapigwa lakini inaokolewa.

Dakika ya 2: Mchezo umeanza kwa kasi ya kawaida.

Mwamuzi anaanzisha mchezo.

Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mchezo unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa, kiungo wa Simba, Jonas Mkude ni mmonja wa wachezaji wanaoanza katika kikosi cha Simba.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI








0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post