PASI YA SAMATTA YAWAONDOSHA GENK KWENYE AIBU YA KICHAPO





Mchezaji huyo wa kimataifa wa Tanzania aliiwezesha timu yake Genk kupata pointi moja kwa kutoa pasi ya bao la kusawazisha dhidi ya Royal Excel



Mbwana Samatta alikuwa kwenye kikosi cha kwanza na alicheza dakika zote 90 katika mechi ya Jumamosi KRC Genk ikiendelea kupita katika kipindi kigumu mwanzo wa msimu huu baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Royal katika uwanja wa nyumbani.

Vijana wa Albert Stuivenberg walionyesha kandanda safi dhidi jitihada za timu ya Mircea Rednic na walihakikisha hawapotezi pointi zote tatu, shukrani kwa bao la kusawazisha la Marcus Ingvartsen.

Royal Excel Mouscron walipata goli la kuongoza mnamo dakika ya 42 Dorin Rotariu akifunga kwa guu lake la kulia akiunganisha pasi ya Sebastien Locigno, kupeleka shangwe kwa mashabiki wa timu hiyo ya ugenini.


Mtanzania, Samatta hakuwa na bahati ya kufunga, lakini alikimbia mara zote na mpira, bila ushindani mwingi sana lakini bahati haikuwa upande wake.

Marcus Ingvartsen hakufanya makosa zikiwa zimebakia dakika tisa mechi kumalizika, alifunga akiunganisha pasi matata ya Samatta na kumshinda kipa Logan Bailly kusawazisha dakika ya 81 ya mchezo.

Hiyo ni mechi ya 66 kwa Samatta akiwa na Genk kwenye michuano yote tangu Januari 2016 alipojiunga na klabu hiyo akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Samatta aliyekuwa mchezaji bora wa Africa wa Mwaka 2016 amecheza mechi yake ya 66, 38 akianzia kikosi cha kwanza na 24 akitokea benchi.
 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI








0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post