Erasto Nyoni
KIRAKA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Klabu ya Simba, Erasto Nyoni, wikiendi iliyopita alitolewa uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi
Nyoni ambaye ni mchezaji mkong- w e , amekuwa a k i i t w a m a r a kwa mara kwenye k i k o s i c h a T a i f a Stars na ameelez a k u w a , anajiona kama ana mkosi kutokana na kupata kadi nyekundu za matukio ya kufanana.
Nyoni ambaye ana m u d u kucheza nafasi zaidi ya tano uwanjani amezungumza na Championi Ijumaa, ambapo amesema pamoja na kuwa ni mchezaji mkongwe na mwenye nidhamu ya juu katika kikosi h i c h o anashangazwa kuwa na bahati mbaya ya kukutana na kadi nyekundu hasa kwenye mechi za kirafiki tu za Taifa Stars.
“Kadi nyekundu ya Jumamosi dhidi ya Malawi ni ya pili nikiwa ndani ya kikosi cha Taifa Stars kwenye mechi za kirafiki jambo ambalo limenifanya kufikiria sana jinsi ilivyotokea.
“Huwezi kuamini, kadi yangu ya kwanza nyekundu kuipata nikiwa na Taifa Stars ilikuwa kwenye mchezo wa kirafiki sikumbuki ilikuwa dhidi ya nani lakini kama ilivyokuwa na Malawi na mazingira yenyewe ya ajabu tu.
“Nakumbuka kadi hiyo nilipewa baada ya kumwambia mwamuzi kwamba maamuzi unayotufanyia hayapo sawa kabisa ila Mungu atatulipia, niliposema hivyo alitoa kadi ya njano kisha nyekundu, akanitoa nje.
“Siku hiyo iliniuma sana kwani ‘gemu’ hiyo nilikuwa nacheza kama kiungo namba sita na ilikuwa ni muda mfupi tu baada ya kipindi cha pili kuanza. “Hii ya pili utaona nilipigwa kadi kama ya uonevu au ya hisia za mwamuzi tu maana alidhani nimempiga kiwiko yule mchezaji wa Malawi wakati si kweli.
“Ukiangalia hata kwenye marudio ya runinga unaweza kuona yule jamaa yeye ndiye alinikanyanga mguuni kabla sijaruka kupiga kichwa mpira, lakini hata bila hivyo utaona tangu mwanzo wa mchezo hakuna sehemu ambayo nilicheza rafu hata moja kwa kuwa nilikuwa makini na nilikuwa najaribu kutimiza jukumu langu ili tuweze kushinda. “ W a a m u z i wetu wakati mwingine nao ni binadamu ila kuna makosa ya wazi sana huwa wanafanya kwani ukiangalia pale hata kama ningeruka vipi nisingeweza kupiga kichwa mpira wa kuokoa ukiwa umeweka mikono nyuma au iwe chini.
“Ninachoona pale mwamuzi (Israel Nkongo) tayari naye alikuwa ameshaanza kuchanganyikiwa na gemu na ndiyo maana alitoa hadi maamuzi yale ambayo utaona ni kiasi gani yalikuwa ya ajabu kwani hata kadi ya Mzamiru nayo ilitokana na mihemko ya mwamuzi tu.
“Kikubwa nimshukuru Mungu kwa kutuwezesha kupata hata hayo matokeo maana wakati tunaingia uwanjani kila mmoja wetu alijua tutamaliza mechi mapema tu ila jamaa walikomaa kiasi cha kutufanya tucheze kwa hofu sana.
“Sina rekodi nyingi za kadi nyekundu maana hata ukifuatilia michezo ya klabu ambazo nimewahi kuzichezea utaona kadi nyekundu nyingine niliwahi kupewa nikiwa Azam FC kwenye Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga ambapo pia nilimwambia refa achezeshe kwa usawa aache kutuminya nikajikuta ananipa kadi ya njano kisha nyekundu eti kwa madai nimemtusi jambo ambalo si kweli,” anamaliza Nyoni.
subscribe na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
Post a Comment