Muigizaji maarufu nchini, Abdallah Makumbila maarufu kama Muhogo Mchungu amesema amepania kufanya vema katika shindano la Vipaji vya Sauti linaloendeshwa na Kampuni ya StarTimes Tanzania chini ya Star Media (T) Ltd ikiwezekana akaishi na kufanya kazi nchini China.
Muhogo Mchungu ni kati ya washiriki waliojitokeza katika shindano hilo ambalo washindi wataendelea kutangazwa na kupewa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.
“Nataka kushinda nifanye kazi kimataifa, hivyo naendelea kushindana. Nina imani nitafanya vizuri kwa kuwa nilijiandaa,” alisema.
Zaidi ya Washiriki 250 walijitokeza katika shindano hilo ambalo lile la kwanza, washindi wake wapo nchini China wakiendelea kufanya kazi jijini Beijing.
Kampuni ya StarTimes Tanzania, wikiendi iliyopita, iliendesha zoezi la kusaka washiriki 10 kutoka jijini Dar, watakaoshiriki Shindano la Vipaji vya Sauti ambapo katika usaili huo, zaidi ya washiriki 2500 walijitokeza.
Katika zoezi hilo lililofanyika kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar, watu mbalimbali maarufu walijitokeza akiwemo Muhogo Mchungu.
Ofisa Mahusiano wa StarTimes Tanzania, Samweli Gisayi, amesema usaili huo kwa wakazi wa Dar, umekuja baada ya kuwapata washiriki watano kutoka Zanzibar na watano jijini Mwanza.
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
Post a Comment