Huda ametajwa na klabu yake kama shujaa halisi
Mlinda mlango wa klabu ya ligi kuu ya Indonesia amefariki baada ya kugongana na mchezaji mwenzake uwanjani.
Choirul Huda, mwenye miaka 38, alikimbizwa hospitalini siku ya Jumapili lakini muda mfupi baadae ilitangazwa kwamba amefariki dunia.
Katika taarifa iliyotolewa na tovuti ya klabu yake Persela FC , daktari wa timu Yudistiro Andri Nugroho amesema mchezaji huyo alifariki baada ya kupata madhara makubwa kifuani.
Anasema mgongano huo ulisababisha kushindwa kupumua kwa Huda.Mashabiki wakiomboleza kifo chake
Ameongeza kuwa madaktari walijaribu kuokoa maisha yake bila mafanikio.
Mchezo huo uliisha kwa Persela kuifunga Semen Padang 2-0.
Maelfu ya mashabiki wamefika hospitalini alipofia mchezaji huyo aliyecheza michezo 500 ya ligi kuu kwa klabu yake pekee.
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
Post a Comment