Mbaraka na Samatta walikuwa kwenye kambi ya Taifa Stars ilipojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
KAMA kuna jambo amelinyaka straika wa Azam FC, Mbaraka Yusuph kwa staa wa kimataifa, Mbwana Samatta, anayekipiga Genk ya Ubelgiji, basi ni usmati wa maisha ya kambini na uwanjani.
Mbaraka na Samatta walikuwa kwenye kambi ya Taifa Stars ilipojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
“Kumbe uwezo wa mchezaji hautokani na mazoezi pekee, kuna vitu vingi nyuma ya pazia,” alisema.
“Mfano mzuri nimeuona kwa Samatta jinsi anavyozingatia muda wa mazoezi, ratiba ya kupumzika na kula.
“Niweke wazi tu kwamba ametuacha mbali na si vibaya kuiga anachokifanya.
“Ulaya ni Ulaya tu, kiufundi Samatta yupo vizuri, hivyo huwezi kumfananisha na mimi, kuna mambo amenizidi ndiyo maana nimesema huyo ni changamoto kubwa kwangu.”
Msimu uliopita akiwa Kagera Sugar, Mbaraka alifunga mabao 12, laini hadi sasa msimu huu ana mabao mawili tu, lakini kasema atapambana.like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
Post a Comment