Man City ilifunga mara tatu katika kipindi cha kwanza na walitawala mchezo kwa asilimia 83.5 katika kile kilichotajwa kuwa mchezo uliolemea upande mmoja
.
Kiungo wa kati wa Ubelgiji walionyesha mchezo mzuri huku Manchester City ikiicharaza Stoke City mabao 7-2 na kufungua uongozi wa pointi mbili katika kilele cha ligi ya Uingereza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa iaka 26 pia alitoa pasi tatu ambazo ziliwekwa wavuni mbali na pasi bora zaidi msimu huu na kusababisha kufungwa kwa bao la pili huku kikosi hicho cha Pep Guardiola kikirudi kutoka mechi za kimataifa na kuwafurahisha mashabiki wa nyumbani na mchezo mzuri.
City ilifunga mara tatu katika kipindi cha kwanza na walitawala mchezo kwa asilimia 83.5 katika kile kilichotajwa kuwa mchezo uliolemea upande mmoja.
Gabriel Jesus alikuwa wa kwanza kucheka na wavu.
De Bryune aliyetoa pasi hiyo baadaye alitoa pasi nyingie kwa Leroya Sane ambaye alimpatia Raheem Sterling na kuweza kufunga.
Ilikuwa 3-0 kufikia dakika ya 27 wakati kiungo wa kati wa Uhispania David Silva kufunga baada ya kazi nzuri kutoka kwa Sterling na Sane.
Na baadye Stoke City ilifunga mabao 2 huku Man City ikiongeza mabao manne.
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
Post a Comment