Liverpool wamepata ushindi mkuwa mno katika historia yao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa walipoifunga saba Maribor kukwea kileleni mwa kundi E
Katika usiku wa Jumanne imekuwa mara ya kwanza Liverpool kufunga idadi ya mabao 5 katika mechi ya ugenini katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, michezo yao 45 iliyopita ya Ligi ya Mabingwa hawakuwahi kufanya hivyo.
Robert Firminho (4), Phellipe Coutinho (13) na Mohamed Salaah (19,40) waliufanya mchezo uende mapumziko huku Liverpool wakiongoza kwa mabao 4 kabla ya Firmninho kuweka la tano kipindi cha pili.
Lakini bao la 6 la Oxlade Chamberlain liliwafanya kuwa klabu ya pili Uingereza kuwahi kufunga mabao 6 katika mchezo wa ugenini ya Ligi ya Mabingwa rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Manchester United huku ikiwa timu ya 9 kufanya hivyo.
Na bao la 7 la Alexander Arnold likawafanya Liverpool kuwa timu ya nne kuwahi kufunga jumla ya mabao 7 na zaidi ambapo timu za Bayern Munich, Barcelona na Lyon zimewahi kufanya hivyo na isitoshe kwa usiku wa leo Liverpool ilikuwa timu pekee ambayo haikuruhusu bao.
Matokeo mengine yaliifanyia upendeleo Liverpool kwani Spartak Moscow waliishangaza Sevilla kwa kichapo cha 5-1 kuwawezesha Reds kupaa hadi kileleni mwa kundi E, pointi moja tu sasa inazitenga timu hizo tatu.
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
Post a Comment