LISSU:WATANZANIA WAJIANDAE KUNIPOKEA,NITASIMAMA TENA



Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, wakiwa na Tundu Lissu hivi karibuni hospitalini Nairobi anakoendelea kutibiwa.
Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia tiketi ya Chadema, Joseph Mbilinyi, amesema ameagizwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kuwaambia wakazi wa Mbeya na Watanzania kwa jumla kuwa wajiandae kumpokea. Hii inafuatia Mbilinyi na mbunge mwenzake wa Chadema, Peter Msigwa, kumtembelea Lissu anayetibiwa katika hospitali moja jijini Nairobi, Kenya ambako wabunge hao walisema afya yake inaendelea kuiamrika.



Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (kulia) akizungumza na Lissu.

Lissu alikimbizwa katika hospitali hiyo baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu ambao mjini Dodoma Septemba 7 mwaka huu.

“Nimemtembelea ‘Big hommie’, Nairobi Hospital. Ameniambia nikawaambie wana-Mbeya kuwa alisikia mwitikio wao wa kishindo nilipomtaja kwenye jukwaa la muziki na kuwa mwili wake ‘uliovunjwavunjwa’ kwa risasi unazidi kuimarika na atasimama tena. Ameniagiza niwaambie wana-Mbeya na Watanzania wote wajiandae, wajiandae, wajiandae” ameandika Mbilinyi kwenye ukurasa wake wa Instagram.
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI








0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post