LIFAHAMU BAO BORA ZAIDI DUNIANI KWAMUJIBU WA FIFA




Bao alilolifunga mchezaji wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Olivier Giroud dhidi ya Crystal Palace
limeshinda tuzo ya Bao Bora la Fifa mwaka 2017, maarufu kama Tuzo ya Puskas.

Alifunga bao hilo siku ya Mwaka Mpya katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Kwenye bao hilo maarufu kama 'scorpion kick', Giroud aliufikia mpira kutoka kwa mshambuliaji Alexis Sanchez kutoka nyuma yake akaupiga kwa mguu wake wa kushoto na kuupitishia juu ya bega kisha ukaugonga mwamba wa goli kabla ya kutulia kimiani.

Bao hilo la Giroud lilipata kura 36.1% kati ya jumla ya kura 792,062 zilizopigwa.

Giroud alikuwa anashindania tuzo hiyo na Deyna Castellanos wa Venezuela na kipa wa Afrika Kusini Oscarine Masuluke.
Kipa bora zaidi

Mshindi wa Kombe la Dunia na mshindi wa Serie A mara 10 Gianluigi Buffon ndiye mshindi wa tuzo ya mlindalango bora duniani mwaka huu.

Aliwasaidia Juventus kushinda taji la ligi mara ya sita mtawalia msimu uliopita.

Aidha, alicheza dakika 600 Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya bila kufungwa.

Buffon, 39, amewashinda kipa Keylor Navas, wa Real Madrid na Manuel Neuer wa Bayern Munich.

"Ni heshima kubwa sana kwangu kupokea tuzo hii katika umri wangu huu," alisema Buffon.


 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI








0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post