Kocha Msaidizi wa Yanga Awaahidi Mashabiki wa Timu Hiyo Kutetea Ubingwa Msimu Huu
Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa “Fusso” amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaahadi kutetea ubingwa wao msimu huu.
Yanga ipo mjini Tabora ikijiandaa na mchezo wake dhidi ya Stand United utakaopigwa Jumapili ijayo mjini Shinyanga.
Juzi timu hiyo ilitoka suluhu na Rhino Rangers katika mchezo wa kujipima nguvu uliopigwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Fusso alisema awaangalia mchezo moja moja wa Ligi Kuu kwani wao kila mchezo kwao ni muhimu katika safari yao ya kutetea ubingwa.
“Siwezi kuzungumzia mchezo mmoja wa Stand United na wakati tuna mechi nyingi tu za Ligi Kuu hivyo sisi tumejipanga kushinda mechi zote ili malengo tuliyojipangia yatimie,”alisema Fusso.
Alisema mashabiki wa soka wasipate hofu kwani chama lao lina wachezaji wazuri wenye kiwango kikubwa ambao wataweza kutetea ubingwa msimu huu.
“Tumejipanga imara tuna wachezaji wazuri na wenye morali hivyo tuko katika mapambano na mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi tutabeba tena Kombe”alisema Kocha huyo Msaidizi.
Yanga ina pointi 12 ikiwa katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu mpaka sasa. like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
Post a Comment