Simba ambao ndiyo wenyeji wa mchezo huo wamedhamiria kuendeleza wimbi la ushindi kama ilivyojuwa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Stand United
Kikosi cha Simba Jumapili kinashuka uwanja wa uhuru Dar es Salaam, kuwakaribisha Mtibwa Sugar, ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa sita Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Timu hizo mbili zinakutana zikiwa zinafanana kwa pointi zote zikiwa katika nafasi ya kwanza na pointi 11 katika mechi tano walizocheza.
Simba ambao ndiyo wenyeji wa mchezo huo wamedhamiria kuendeleza wimbi la ushindi kama ilivyojuwa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Stand United.
Mchezo huo hautarajiwi kuwa rahisi kwa pande zote mbili ingawa wenyeji Simba wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na ubora was kikosi walichokuwa nacho msimu huu ambacho kimesheheni nyota wenye majina makubwa yofauto na kile cha wapinzania wao.
Koch wa Simba Joseph Omog, amesema anatambua ugumu was mchezo huo lakini amekiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha wanaibuka na ushindi ili kuenelea kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.
"Natambua Mtibwa ni timu nzuri na ngumu lakini maandalizi ya wiki nzima tuliyofanya baada ya mapumziko ya timu za taifa yameturudisha kwenye shepu yetu na sasa tupo tyari kwa mchezo wa kesho," amesema Omog.
Mkameruni huyo amesema amezungumza na wachezaji wake na kuwaeleza umuhimu wa ushindi katika mchezo huo hivyo anaamini kazi kesho itafanyika na baada ya dakika 90 Simba ndiyo wataibuka kifua mbele.
Kwa upande wake kocha mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila, amesema anaiheshimu sana Simba kwasababu ni timu nzuri inaongoza ligi lakini hawapo tayari kupoteza mchezo huo.
Katwila amesema wamepanga kutumia mfumo wao wa 4-4-2 ambao waliutumia kwenye mchezo dhidi ya Yanga na kupata matokeo mazuri.
Katwila amesema ataendelea kuwatumia wachezaji wake Mohamed Issa na kiungo mshambuliaji Hassan Dilunga pamoja na Stamili Mbonde ambao ameahidi kuwaanzisha kwenye kikosi cha kwanza.
"Nazijua vyema njia nyingi ambazo zimekuwa zikiwapa Simba ushindi na mimi nimewaelekeza wachezaji wangu nikiamini kama watazifuata vizuri tunaweza kuwadhibiti na kuwafunga pia," amesema Katwila.
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
Post a Comment