HAYA NDO MAHOJIANO YA RONALDO NA FIFA





Cristiano Ronaldo alitajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa FiFA kwa mara ya pili mfululizo jana jijini London, na nahodha wa Ureno jana baada ya kumalizika kwa shughuli ya ugawaji wa tuzo alifanya mahojiano na FIFA.



FIFA.com: Cristiano Ronaldo, hii ni awamu ya pili ya ufanyikaji wa tuzo za The Best FIFA Football Awards, na ni mara ya pili unashinda, unajisikiaje?


Cristiano Ronaldo: Ni kitu kikubwa kwangu. Ningependa kuwashukuru wachezaji wenzangu. Ni hatua kubwa kwenye maisha yangu ya soka, ninajisikia furaha sana.

Hii ni mara ya tano unapata heshima ya kuwa mchezaji bora kabisa wa soka, je heshima hii inakufanya kuwa miongoni mwa wachezaji bora kuwahi kutokea?
Nina furaha sana kushinda hii tuzo leo, lakini kitu nilichotaka tangu mwanzo ni kuwa na mafanikio katika huu mchezo na nashukuru nimefanikisha hilo. Kushinda makombe na kuwa miongoni mwa wachezaji tuzo nyingi binafsi ni jambo la kujivunia sana. Ni vitu ambavyo siwezi kusahau kwenye maisha yangu na vinazidi kunipa msukumo wa kujituma kwa kadri ninavyoweza.



Hivi karibuni umepata mafanikio ya kutwaa taji kubwa ukiwa na timu yako ya taifa ya Ureno, ushindi wa Euro 2016 na kuelekea fainali za kombe dunia 2018 nini mategemeo yako?


Ushindi wa wa EURO 2016 ulikuwa muhimu, kombe kubwa ngazi ya kimataifa ndio kitu kilichokuwa kinamiss kwenye kabati langu la mafanikio. Nashukuru mwaka huu tumefuzu na tunajiandaa kwenda Russia tena.

Tuizungumzie Russia, nchi ambayo uliitembelea wakati wa mashindano ya FIFA Confederations Cup.

Tayari nimeshacheza Urusi mara nyingi. Nimeshinda ubingwa wa Champions League kule, ni nchi ambayo nina bahati nayo. Lakini bahati haikuwa yetu, tulishindwa kushinda taji la Kombe la mabara, lakini nilipata uzoefu mpya.

Baada ya ushindi wa UEFA EURO 2016, baadhi ya wachambuzi wamekuwa wakiipa nafasi Ureno kutwaa kombe la dunia. Unakubaliana na utabiri wao?


Hilo linaeleweka. Sisi ni mabingwa watetezi wa ulaya na hilo bila shaka linaongeza mategemeo, lakini ningependa kurudia nilichosema kabla ya EURO 2016: Ureno sio timu ambayo huwa inapewa nafasi ya kufanya vizuri kwenye mashindano makubwa. Kuna timu nzuri zaidi yetu ukiangalia kwenye ukubwa wa kikosi, na mafanikio waliyonayo. Hivyo sisi tutaingia huku tukifahamu hilo, japokuwa tutajitahidi kufanya vizuri.



Umeshashinda tuzo 5 za uchezaji bora wa dunia. Ungependelea kumaliza na ngapi katika maisha yako ya soka?
7, ningependelea kushinda idadi hiyo, 7 ndio namba yangu ya bahati. Lakini hayo yote yapo kwenye wakati ujao, kwa sasa nitaendelea kujituma na kufurahia matunda ya jitihada zangu.

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI








0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post