Antonio Conte aliteuliwa meneja wa Chelsea Aprili 2016
Meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte amepuuzilia mbali madai kwamba kuna mtafaruku katika klabu hiyo kutokana na mfumo wake wa mazoezi.
Taarifa zimekuwa zikisema wachezaji wa klabu hiyo wamechoshwa na mazoezi makali wanayolazimishwa kuyafanya na Conte.
Hata hivyo, Mwitaliano huyo amesema mazoezi anayowafanyisha msimu huu ni "70% chini" ya mazoezi aliyowafanyisha msimu uliopita ambapo walishinda Ligi ya Premia.
"Sina habari kuhusu haya," amesema meneja wa Juventus Conte, alipoulizwa kuhusu uvumi huo kwenye vyombo vya habari.
Chelsea wamecheza mechi tatu bila kushinda hata moja mechi zao za karibuni zaidi.
Walishindwa na Manchester City na Crystal Palace Ligi ya Premia kabla ya kutoka sare 3-3 nyumbani dhidi ya Roma Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano.
Jumamosi, Chelsea, ambao wamo alama tisa nyuma ya viongozi Manchester City, watakuwa wenyeji wa Watford.
Itakuwa mechi yao ya tatu katika siku saba.
Msimamo wa ligi ya EPL 2017/18
Inter Milan wanamtafuta Antonio Conte?
Conte anaamini kucheza mechi nyingi - pamoja na kukosa muda wa kujiandaa - vimechangia kudorora kwa uchezaji wao.
"Unapocheza kila siku tatu ni vigumu kufanyia kazi mbinu zako za kiufundi na pia hali ya wachezaji," ameongeza.
"Nafikiri sasa hatuangazii zaidi uchezaji kwa kina."
Shinikizo kwa Conte?
Chelsea hawajashindwa mechi tatu mfululizo Ligi ya Premia tangu wiki za mwanzo wa msimu wa 2015.
Jose Mourinho, aliyekuwa ameshinda taji la ligi 2014-15, alifutwa wiki chache baadaye.
Alipoulizwa iwapo anahisi presha, Conte ameongeza: "Nafikiri kila kocha, kila meneja lazima ahisi presha.
"Ninapokwenda nyumbani kwangu huwa nina furaha kwa sababu najua kila wakati huwa najitoleza kabisa katika kazi yangu kwa klabu hii, mashabiki na wachezaji wangu.
"Lakini mwajua vyema kwamba lolote laweza kutokea katika soka."
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
Post a Comment