ARSENAL WACHEZEA KICHAPO 2-1 KWA WATFORD


Watford wameruka hadi nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Vicarage Road.
Per Mertesacker aliipa Arsenal uongozi  lakini goli la penati kutoka kwa Troy Deeney na lile la ushindi la dakika za mwisho la Tom Cleverley imewafanya Watford kuibuka na ushindi wa kwanza nyumbani dhidi ya Gunners tangu 1987.
Arsene Wenger amesema kuwa Watford haikupaswa kupewa penati  kwani Richarlison ameanguka kirahisi sana , lakini wageni hao wamefungwa kwa mara ya kwanza baada ya mechi nane za mashindano yote 
Timu zote mbili ziliingia katika mchezo huo kwa imani kubwa ya kuibuka na ushindi kutokana na klabu zote kuwa na matokeo mazuri hivi karibuni/
Ilichukua mpaka dakika ya 19 kwa klabu kutengeneza nafasi, kwa Abdoulaye Doucoure kupiga krosi murua iliyomkuta Roberto Pereyra, ambaye alipiga kichwa kilicho paa juu ya lango.
Arsenal ilihitaji karibu nusu-saa ili kupata nafasi yao ya kwanza kwenye lango la Watford, kwa Mohamed Elneny kupiga shuti la umbali la mita 25 ambalo liligonga mwamba. 
Hata hivyo, baada ya nusu saa ya mchezo huo, Gunners walitawala mechi hiyo kwa kiasi kikubwa na dakika sita kabla ya kipindi cha kwanza kuisha, Arsenal walikuwa mbele kwa goli moja.
Kona ya Granit Xhaka ilitua kichwani kwa Mertesacker aliyekuwa kwenye yadi ya sita, na mlinzi huyo hakujiuliza mara mbili ili kufunga bao lake la kwanza la Ligi Kuu baada ya miaka minne.
Arsenal ilitawala kipindi cha kwanza, huku Xhaka akizuiliwa nafasi yake na mlinda mlango wa Watford, Heurelho Gomes kabla Hector Bellerin ajapiga shuti la mguu wa kushoto lililopita karibu na lango.
Watford ilibadilika baada ya kuingia kwa Richarlison iliongeza mashambulizi mengi kwa upande wao,Kabla ya saa ya mchezo,
Nyota wa Arsenal Danny Welbeck alitolewa nje na nafasi yake ilichukuliwa na Mesut Ozil na hakuchukua muda Mjerumani huyo akamtengenezea nafasi Alex Iwobi ambaye mpira wake uliokolewa na Gomes.
Ozil kidogo aipatie goli la pili Arsenal  baada ya kujikuta mwenyewe  katika eneo la kumi na nane lakini mchezaji huyo shuti lake lilishindwa lenga goli kwa ustadi.
Baada ya Arsenal kukosa nafasi ya wazi ,Watford walifanikiwa kupata penati.  baada ya Bellerin kumpiga kikumbo Richarlison ndani ya eneo la hatari na Deeney hakufanya kosa kwa kumtuma Petr Cech njia isiyofaa na kuwa goli lake la kwanza la ligi katika mechi 14.
Dakika kumi za mwisho kidogo Etienne Capoue aipatie timu yake goli la pili wakati risasi yake kali ilipongonga mwamba baada ya kumgusa Mertesackert.
Hata hivyo, katika dakika za nyiongeza, Watford walifanikiwa kupata goli lake la ushindi kupitia kwa Cleverley, 
Gunners sasa wako nyuma kwa  pointi tisa dhidi ya vinara wa Ligi Kuu, Manchester City.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI








0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post