Josep Maria Bartomeu amesisitiza mara kadhaa kuwa ni swala la muda tu tangazo litatolewa, lakini Iniesta anataka tetesi zikome mara moja.
Andres Iniesta amewataka viongozi wa Barcelona kuhakikisha Lionel Messi anasaini mkataba mpya kwani klabu "haiwezi kuishi bila yeye".
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina bado hajajifunga rasmi na miamba wa Catalan, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kufika tamati mwishoni mwa msimu.
Rais wa Barca Josep Maria Bartomeu amesisitiza mara kadhaa kuwa ni swala la muda tu tangazo litatolewa, lakini Iniesta - ambaye binafsi amesaini Ijumaa mchana anataka tetesi zikome kabisa.
"Kwa swala la Leo nadhani hakuna shida katika swala la mazungumzo," aliwaambia waandishi. "Klabu inamhitaji Leo, anahitaji kuwa hapa. Natumai habari zake [katika Barca] hazitakoma.
"Ni wa kipekee, hatuwezi kuishi bila yeye na nadhani klabu inafikiri namna hiyo hiyo. Ni wala la muda tu, lakini natumai atasaini mkataba mpya mapema iwezekanavyo."
Iniesta amefuta shaka zote juu ya mustakabali wake Barcelona baada ya kukubali kusaini mkataba wa "maisha" Camp Nou.like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika
For Booking>>>
EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
Post a Comment