Klabu za Ligi Kuu ya England ziliweka rekodi mpya ya kutumia pesa nyingi zaidi siku ya mwisho ya kuhama wachezaji, ambapo jumla ya £210m zilitumiwa.
Licha ya klabu za Ligi ya Premia kutumia £1.4bn kipindi chote cha kuhama wachezaji- ambayo ni rekodi mpya - Alexis Sanchez, Virgil van Dijk, Riyad Mahrez, Thomas Lemar, Diego Costa na Ross Barkley bado hawakufanikiwa kuhama.
Siku ya mwisho ya kuhama wachezaji msimu uliopita ilikuwa £155m.
Chelsea walitumia £35m kumnunua Danny Drinkwater naye Mamadou Sakho akanunuliwa £26m na Crystal Palace kutoka Liverpool, taarifa za kuhama kwao zikitangazwa baada ya muda rasmi wa kuhama wachezaji.
Wawili hao ndio waliosaidia kuvunja rekodi ya mwaka jana.
Chelsea walinunua pia Davide Zappacosta, Spurs wakamchukua mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente kwa £15m, klabu hiyo ya Wales nayo ikajaza nafasi hiyo kwa kumchukua Wilfried Bony kwa £12m.
Philippe Coutinho, ambaye Barca waliwasilisha £114m mapema Agosti kutaka kumchukua mapema Agosti lakini ombi lao likakataliwa, amesalia kuwa mchezaji wa Liverpool lakini bado anaweza kuhama kwani dirisha la kuhama wachezaji Uhispania litafungwa saa saba usiku Ijumaa.
Wachezaji waliothibitishwa kuhama awali Alhamisi walikuwa:
•Kylian Mbappe [Monaco - PSG] Mkopo, ambapo baadaye anaweza kununuliwa £165.7m
•Alex Oxlade-Chamberlain [Arsenal - Liverpool] £35m
•Serge Aurier [PSG - Tottenham] £23m
•Renato Sanches [Bayern Munich - Swansea] Mkopo
•Nikola Vlasic [Hajduk Split - Everton] £10m
Jumla ya £1.4bn zilizotumiwa na klabu za Ligi ya Premia msimu huu zinazidi rekodi ya msimu uliotangulia ya £1.120bn na ni karibu £1bn zaidi ya pesa zilizotumiwa miaka mitano iliyopita.Takwimu kuhusu Leicester zinajumuisha ununuzi unaotarajiwa wa Adrien Silva Ijumaa
Licha ya Manchester City kushindwa kumchukua Alexis Sanchez na beki wa West Brom Jonny Evans, vijana hao wa Pep Guardiola ndio walioongoza kwa kutumia £215m ambapo wanazidi klabu nyingine yoyote ile.
Paris St-Germain walivunja rekodi kwa mchezaji binafsi kwa kumchukua Neymar kwa £200m nao Barcelona wakamchukua Ousmane Dembele kwa £135.5m.
PSG wameahidi kutoa £165.7m baadaye kumchukua Kylian Mbappe, ambaye kwa sasa wamemchukua kwa mkopo, kwa mkataba wa kudumu majira ya joto mwaka ujao.
Wachezaji ambao hawakuhama
Rekodi iliyowekwa ingekuwa juu zaidi kwa £200m - iwapo baadhi ya wachezaji wa thamani ya juu ambao walitarajiwa kuhama wangefanikiwa.Alexis Sanchez alichezea Chile saa chache baada ya uhamisho wake kwenda Manchester City kutibuka
Sanchez wa Arsenal alikaribia kuhamia kwa Manchester City kwa £55m. Lakini mkataba huo ulitegemea Lemar kujiunga na Gunners kujaza nafasi yake. Arsenal walikuwa wamekubaliana na Monaco kumchukua kwa £90m, uhamisho ambao ungemfanya wa tatu kwa thamani, lakini mchezaji huyo wa Ufaransa alikataa kuhama na hivyo Sanchez naye akakwama.
Kiungo wa kati wa Everton Barkley, ambaye kwa sasa amejeruhiwa, alikataa kuhamia Chelsea kwa£30m - hata baada ya kudaiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. Barkley amesalia na mwaka mmoja Everton na hatatia saini mkataba mpya.
Beki wa Southampton Van Dijk amekuwa akifanya mazoezi ya timu ya vijana ya klabu hiyo tangu alipoanza kujaribu kulazimisha kuhamia Liverpool. Lakini hilo halikufanikiwa, hivyo atasalia St Mary's.
Mshambuliaji wa Chelsea Costa anaaminika kuwa nchi yake ya kuzaliwa ya Brazil baada ya kuambia hayupo katika mipango ya meneja Antonio Conte. Lakini hakuhama. Hali isipobadilika, hataweza kucheza kwa kipindi cha hadi miezi minne.
Winga wa Leicester Mahrez aliruhusiwa kusafiri Ulaya na timu ya taifa ya Ulaya kukamilisha uhamisho wake, lakini yamkini hakuna aliyefanya juhudi za kumsajili. Roma walikuwa wametaka kumnunua lakini dau zao zikakataliwa mara kadha awali.
Manchester City waliacha kumtafuta beki wa West Brom Evans baada ya kushindwa kumuuza Eliaquim Mangala kwa Crystal Palace.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya England ya vijana wa chini ya miaka 17 Jadon Sancho alihamia Borussia Dortmund kutoka Manchester City kwa £10m, ambapo alipewa jezi nambari saba ya Ousmane Dembele.
Chipukizi mwingine wa England alihamia Ujerumani, Liverpool walimkabidhi Ryan Kent kwa mkopo kwa Freiburg.
Liverpool pia walimkabidhi Divock Origi kwa Wolfsburg kwa mkopo.
Klabu ya Harry Redknapp Birmingham alivunja rekodi ya klabu hiyo kumnunua winga wa Brentford Jota kwa zaidi ya £6m.
Lazio walimchukua winga wa zamani wa Manchester United Nani kutoka Valencia kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Stoke City walimtuma Giannelli Imbula (Toulouse) na mshambuliaji Bojan Krkic (Alaves) kwa mkopo kwa msimu mmoja.
Arsenal walimkabidhi Lucas Perez kwa Deportivo La Coruna kwa mkopo, mwaka mmoja baada ya kulipa kiasi sawa kwa klabu hiyo £17.1m kumchukua.
Kiungo wa kati wa England Ravel Morrison aliondoka Lazio na kwenda klabu ya Atlas ya Mexico.
Post a Comment