UHONDO wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba ni keshokutwa Jumatano. Hii itakuwa ni mechi ya nne timu hizo kukutana katika michuano hiyo lakini mechi hii inatarajiwa kuwa kivutio kikubwa zaidi kutokana na usajili ulivyofanyika.
Michuano hii ya Ngao ya Jamii, kwa kawaida huwa ni ‘Super Cup’, kwa maana ya kukutanisha mabingwa wa michuano miwili tofauti (au bingwa wa FA vs mshindi wa pili wa ligi kama bingwa wa ligi na FA ni yuleyule) lakini kwa muda mrefu kwa Bongo imekuwa ikimkutanisha mshindi wa kwanza na wa pili wa ligi kuu kwa kuwa hatukuwa na Kombe la FA, hivyo kukosa mantiki.
Safari hii kuna uhalisia zaidi, watu wataona nani mkali kati ya bingwa wa ligi kuu (Yanga) na wa Kombe la FA (Simba). Kwa Tanzania, hii ni itakuwa ni mechi ya 10 ya Ngao ya Jamii, tangu ilivyoanzishwa mwaka 2001, kisha ikafa na kuja kuibuka tena baada ya miaka nane.
YANGA YACHEZA MARA NYINGI ZAIDI YA SIMBA
Yanga ndiyo timu ambayo imecheza mechi nyingi zaidi za Ngao ya Jamii tangu ilivyoanzishwa mwaka 2001 kati ya timu nne ambazo zimewahi kucheza mechi hiyo.
Hadi sasa ina jumla ya mechi nane ambazo imecheza dhidi ya Simba mara (3), Mtibwa mara (1) na Azam mara (4).
Simba imecheza michuano hii mara nne dhidi ya Yanga mara (3) na dhidi ya Azam mara (1). Azam wamecheza mara tano mfululizo kuanzia 2012, dhidi ya Simba mara (1) na dhidi ya Yanga mara (4). Mtibwa ni mara moja dhidi ya Yanga.
YANGA YATWAA NGAO 5, SIMBA 2
Yanga imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii mara tano zaidi ya Simba ambayo imechukua mara mbili tangu ilipoanza kushiriki.
Simba.
YANGA 5, SIMBA 4
Yanga imefani kiwa kuifunga Simba jumla ya mabao matano katika Ngao ya Jamii pindi ilipokutana katika miaka tofauti ambapo mwaka 2001, Wanajangwani hao waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na mwaka 2010 waliifunga penalti 3-1. Lakini Simba imewafunga wapinzani wao hao jumla ya mabao manne yakiwemo mawili kwenye ushindi wa 2-0 mwaka 2011.
WAFUNGAJI SIMBA, YANGA ZILIVYOKUTANA
Yanga 2-1 Simba (2001)
Mabao ya Yanga yalifungwa na Edibily Lunyamila na Ally Yusuph ‘Tigana’ la Simba lilifungwa na Steven Mapunda.
Simba 1-3 Yanga (2010) penalti
Penalti ya Simba ilifungwa na Mohamed Banka huku Emmanuel Okwi na Uhuru Seleman wakikosa penalty, na kwa upande wa Yanga zilipigwa na Godfrey Bonny, Stephano Mwasyika na Isack Boakye.
Simba 2- 0 Yanga (2011)
Wafungaji Haruna Moshi ‘Boban na Felix Sunzu.
AZAM MECHI 5, IMECHUKUA MARA MOJA
Azam ndiyo timu yenye historia ya kucheza Ngao ya Jamii mara nyingi zaidi na kushindwa kuchukua kombe hilo . Azam wamecheza mara tano kwenye mechi hizo na kufanikiwa kushinda mara moja pekee.
MT IBWA SUGAR NAO WAMO
Mtibwa Sugar ya Morogoro nayo iliwahi kuonja raha ya ushindi wa mchezo huu, kwani iliifunga Yanga bao 1-0 mwaka 2009.
Post a Comment