Uongozi wa Klabu ya Simba, umeamua kuwasamehe wanachama 71 wa timu hiyo kutoka Tawi la Simba Maendeleo maarufu kwa jina la Simba Ukawa na kuwarejesha kundini huku ukiwataka kufuta kesi yao waliyoifungua mahakamani.
Kundi hilo la wanachama 71, lilifutwa uanachama na uongozi uliopo madarakani chini ya Rais Evans Aveva, kutokana na kwenda kufungua kesi mahakamani wakipinga kufanyika kwa uchaguzi ikiwa ni kinyume na Katiba ya Simba.https://edusportstz.blogspot.com/
Azimio la kuwarejesha kundini wanachama hao wa Simba Ukawa liliazimiwa na wanachama wengine wa klabu hiyo kwenye mkutano mkuu uliofanyika jana Jumapili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar.
Katika mkutano huo ulioendeshwa na Kaimu Rais wa Simba, Salum Abdallah ‘Try Again’ ambapo kwa umoja wao waliwasamehe wanachama hao huku wakiwapa sharti la kwenda kufuta kesi yao ya msingi ambayo waliifungua.
“Wakishafuta kesi hiyo na kamati yetu ya utendaji ikajiridhisha basi hatutakuwa na budi kuwarejesha rasmi kwenye timu yetu na kuungana pamoja baada ya kupita muda tangu tulipowafungia,” alisema Salim.
Post a Comment