MO DEWJI MBIONI KUKABIDHIWA SIMBA FC


Hali ilivyo ukumbini hapo.






Maanadalizi ya ya mkutano huo.



Wanachama wa Klabu ya Simba wakijiandaa kwa ajili ya mkutano huo.


Kwa mara nyingine tena, Wanachama wa Klabu ya Simba wamekutana kufanya Mkutano Mkuu wa Klabu leo Jumapili kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyarere International Conference Centre) jijini Dar es Salaam.



Ukumbi huo wa kisasa kabisa nchini upo maeneo ya Ocean Road, jirani na Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM), utakuwa unatumiwa kwa mara ya pili na klabu hiyo baada ya kutumika Jumapili iliyopita.




Wanachama wakijadiliana kabla ya mkutano huo.

Mkutano huo ni mwendelezo wa maandalizi ya Klabu ya Simba kufanya mabadiliko ya kimfumo katika kuiongoza klabu hiyo.


Msemaji wa Simba, Haji Manara akizungumza.

Mmoja wa wanachama maarufu wa Simba, Mohamed Dewji ‘MO’ anatarajiwa kuwa mmoja wa wadau waliopanga kuwekeza baada ya mfumo wa uendeshaji kubadilishwa.



Wanachama ni furaha kwenda mbele.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post