MAAJABU:MVULANA ATUMIA FILAMU KUMUOKOA NDUGU YAKE



Christa O'Connor na wanawe huishi Roseville, karibu na Detroit

Nyota wa Hollywood Dwayne Johnson, almaarufu The Rock amemtaja mvulana wa miaka 10 kuwa "shujaa halisi" baada ya mvulana huyo kutumia mafunzo kutoka kwa filamu kumuokoa ndugu yake.

Jacob O'Connor kakake wa miaka miwili Dylan akielea kwenye kidimbwi cha kuogolea uso wake ukiwa kwenye maji.

Lakini badala ya kukimbia kuomba usaidizi alitumia mafunzo aliyoyapata kutoka kwa filamu aipendayo sana ya San Andreas.

Jacob, kutoka Roseville, Michigan, alifanikiwa kumtoa ndugu yake kutoka kwenye kidimbwi na kuanza kumpa huduma ya kwanza kumsaidia kuanza kupumua tena, kama alivyoona The Rock akifanya kwenye filamu hiyo.

Dylan baadaye alikimbizwa hospitalini na alipata nafuu kabisa.

Aliposikia kuhusu aliyoyafanya Jacob, Dwayne Johnson aliandika kwenye Twitter: "Kisa cha kuvutia sana....wewe ni shujaa halisi. Tunajivunia! DJ."

Mamake Jacob, Christa O'Connor aliambia BBC kwamba alifurahishwa sana na alichofanya Jacob.

"Nilishangaa kwamba alikumbuka alichokuwa ameona kwenye filamu hiyo, ambayo anaipenda sana na alikuwa ameitazama wiki iliyotanguliwa."Jacob (kushoto) alimuokoa kakake kwa kurudia aliyokuwa ameyaona The Rock akifanya kwenye filamu

The specific scene Jacob was copying was one in San Andreas where Johnson's character tries to save his on screen daughter.

Jacob aliambia vyombo vya habari: "Niliingiwa na wasiwasi nilipomuona Dylan kwenye kidimbwi...Nilikumbuka kwenye filamu ya San Andreas, baada ya tetemeko la ardhi, kisha kukatokea kimbunga na msichana alikuwa katika hatari ya kufa maji.

"Katika filamu nyingi, hilo ndilo jambo la kwanza watu hufanya (huduma ya kusaidia mtu kupumua). Jaribu kumuokoa mtu kwanza, na ikiwa hilo halisaidii, basi tafuta usaidizi."Jacob O'Connor na ndugu zake Gavin (kushoto) na Dylan (kati)

Dylan alikuwa amefungua milango miwili ya nyuma na kuingia kwenye bustani na alipokuwa akitembea akatumbukia kwenye kidimbwi cha kuogelea

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post