KOCHA WA YANGA: SIMBA MTOTO TU KWA YANGA




Kikosi cha Yanga SC.

MLAN-DEGE FC hivi karibuni ilifungwa mabao 2-0 na Yanga, halafu ikatoka suluhu na Simba, sasa kocha wa timu hiyo Jaala Abdallah Salum amesema Yanga ipo vizuri kuliko Simba katika fiziki.

Simba na Mlandege zilitoka suluhu usiku wa kuamkia jana Ijumaa katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan ambapo kabla ya mechi hiyo Mlandege ilifungwa mabao 2-1 na Yanga ambayo wafungaji wake walikuwa Ibrahim Ajibu na Emmanuel Martin.


Wachezaji wa timu ya Yanga.

Katika kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii itakayochezwa Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kocha huyo amesema Simba itabidi irekebishe baadhi ya mambo kama inataka ushindi.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Salum alisema timu yake ilitoka sare na Simba kutokana na fiziki yao kuwa juu kuliko wapinzani wao hali ambayo ni tofauti na walipocheza na Yanga.

“Mechi yetu na Simba ilikuwa nzuri kwetu kwani tuliwazidi katika fizikia maana wao ilioneka ipo chini tofauti na sisi, lakini Yanga walitusumbua kwa sababu walikuwa na fiziki kuliko sisi.

“Yanga walikuwa fiti kuliko sisi walikuwa na nguvu na kasi katika muda wote wa mchezo, Kocha wa Yanga George Lwanda-mina ni mjanja sana kwa sababu alianza kuwatumia vijana, wakatu-chosha.

“Halafu akawaingiza wale ambao ni wazoefu ikawa shida kwetu ila kikubwa ilikuwa fizikia yetu ipo chini, nadhani Simba huenda katika siku hizi mbili wakawa vizuri kabla ya mchezo na Yanga vinginevyo itakuwa tabu kwao,” alisema Salum.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post