kikosi cha Liverpool chatajwa huku Philippe Coutinho akiachwa nje


https://edusportstz.blogspot.com/


Liverpool walimnunua Coutinho kutoka Inter Milan kwa £8.5m mwaka 2013

Philippe Countihno ameachwa nje ya kikosi cha Liverpool kitakachoshiriki mechi ya kwanza ya michuano ya muondoano ya kufuzu kwa hatua ya makundi katika ligi ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Hoffenheim leo Jumanne jioni.

Kiungo huyo wa kati, mwenye umri wa miaka 25, aliwasilisha ombi lake la uhamisho wiki iliyopita, siku chache baada ya klabu hiyo kukataa euro milioni 100 (£90m) kutoka Barcelona.

Countinho alikosa kushiriki mechi ya ufunguzi siku ya Jumamosi katika ligi ya Premia dhidi ya Watford kutokana na jeraha la mgongo.

''Hakuna kitu kichobadilika. Si kwa upande huu au ule,'' meneja Jurgen Klopp amesema kuhusiana na raia huyo wa Brazil siku ya Jumatatu.

''Hatuchezei kwa sasa, hilo ndilo suala kubwa mnalotaka kujua. Hawezi kuichezea Liverpool kwa wakati huu na kila mtu anaweza kulitafakari hilo, kwamba ni pigo kwetu.

''Tumefahamu hilo kwa siku chache, kwa hivyo tunaweza kujitayarisha kwa mechi hii bila yeye, kama vile tunajitayarisha bila Adam Lallana na Daniel Sturridge.''
Barca wamekuwa na matamanio ya kumpata Coutinho baada ya kumuuza Neymar kwa klabu ya Paris St-Germain kwa kima kilichovunja rekodi ya dunia cha pauni milioni 200.

Coutinho alisaini mkataba wa miaka mitano mwezi Januari, ambao haukujumuisha kipengee cha kuondoka kwake.

Liverpool wataanza kampeini yao ya Ulaya na hatua ya kwanza ya muondoano katika uwanja wa Rhein-Neckar-Arena nchini Ujerumani na mechi ya amrudiano itakuwa Anfield siku ya Jumatano tarehe 23 mwezi Agosti.

Mshindi atasonga mbele katika hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Ulaya

Kikosi cha Liverpool: Alexander-Arnold, Moreno, Lovren, Milner, Wijnaldum, Henderson, Can, Mane, Salah, Firmino, Kent, Solanke, Origi, Gomez, Klavan, Flanagan, Robertson, Matip, Grujic, Mignolet, Karius na Ward.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post