Ulimboka Mwakisikye ‘Senga’.
MCHEKESHAJI mkongwe, Ulimboka Mwakisikye ‘Senga’ amesema kwa sasa sanaa imekuwa ngumu hivyo kitu pekee kinachomuingizia pesa ni kufanya vichekesho vya majukwaani huko mikoani pamoja na kualikwa kwenye shughuli mbalimbali za kijamii hivyo kulipwa chochote kidogo ili kuyasongesha maisha.
Akipiga stori na mwandishi wetu hivi karibuni kupitia simu ya mkononi, Senga ambaye alidai yupo wilayani Kahama, Shinyanga kufanya shoo, alisema kuwa, imebidi kubadili maisha badala ya kusubiri tenda za filamu hivyo amekuwa akisafiri mikoa mbalimbali ambako kuna soko kubwa la sanaa ya uchekeshaji.
“Maisha yamebadilika sana, kama msanii ukitegema dili za filamu, utaua watoto kwa njaa, lazima utoke kuhangaika, mimi na mwenzangu, Pembe tunatumia fursa ya kwenda mikoani kufanya shoo za majukwaani na kupata mialiko ya sherehe mbalimbali za watu na kupewa pesa,” alisema Senga
Post a Comment