Msemaji Machachari aliyefungiwa wa klabu ya Simba Haji Manara, ametoa ya Moyoni kuwa
kuwa hajapendezeshwa timu ya Everton inayotokea Uingereza kuondoka nchini bila ya kucheza na klabu ya Simba na Yanga.
Manara ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram muda mchache ulipomalizika mchezo wa kirafiki baina ya Everton dhidi ya Gor Mahia ya Kenya mtifuano ulichezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaama jana Jioni.
"Sijapenda kwa Klabu zetu mapacha kukosa nafasi ya kucheza na kina Rooney, ila Mungu ni fundi maana wangepata nafasi wale jamaa wangejiita wa mbinguni, jina la wakimataifa wangeliacha", ameandika Manara.
Katika hatua nyingine, timu ya Everton ilifanikiwa kuwachapa Gor Mahia kwa mabao 2-1 ambapo ndani ya dakika 34 za kipindi cha kwanza Rooney aliweza kupachika bao la kwanza lakini ilipofika dakika ya 36 bao hilo lilisawazishwa na Tusiyenge mchezaji kutoka Gor Mahia.
Kama hiyo haitoshi ilipofika dakika 80 kipindi cha pili Everton waliongeza bao la pili kupitia mchezaji wake Dowell na kupelekea mpaka kinapulizwa kipenga cha mwisho Everton kuwa mbele kwa mabao 2-1 na kuifanya timu hiyo kuwa mshindi
Post a Comment