Umesikia alichokisema Masau Bwire kuhusu Simba?


Mara baada ya ratiba ya Ligi Kuu Bara kutolewa juzi Jumatano huku klabu ya Ruvu Shooting ya Pwani itaanza na Simba, katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo, Msemaji wa Ruvu, Masau Bwire, amesema hawaogopi kucheza na wapinzani wao hao.

Masau alisema wapinzani wao Simba hawajasajili wachezaji bali wamesajili majina ya wachezaji na wana furaha kuanza nao katika mchezo wao wa kwanza.

“Kwanza niseme tuna furaha ya kuanza na timu kubwa kwa sababu tunataka tuuonyeshe ulimwengu kuwa sisi ni nani, najua kuwa wapinzani wetu wamesajili wachezaji wakubwa wenye majina makubwa.

“Lakini niwaambie mashabiki kuwa, Simba hawajasajili wachezaji, bali wamesajili majina ya wachezaji na siku hiyo tutawaonyesha utofauti wa wachezaji na majina,” alisema Masau.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post