Viongozi wa kimataifa, wanaharakati wakerwa na uamuzi wa Trump


Chansela Angela Merkel
Viongozi wa Ulimwengu na makundi ya wanaharakati wa mazingira wameeleza kukerwa kwao na uamuzi wa Rais Donald Trump kujitoa katika mkataba wa hali ya hewa wa Paris.

Mkataba huo wa kihistoria ni juhudi kubwa za kimataifa zilizochukuliwa katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema katika lugha zote mbili Kifaransa na Kiingereza kwamba anaamini Trump amefanya kosa la kihistoria.

Macron amesema wanasayansi wa Kimarekani na wajasiriamali watatambua sasa kuwa Ufaransa ni makazi yao ya pili,”akiwakaribisha kuishi Ufaransa ambako wanaweza “kufanya kazi pamoja katika kutafuta suluhu kamili ya hali ya hewa yetu, mazingira yetu.”

Macron ameongeza kuwa wakiwa Ufaransa watafanya kazi “kuifanya dunia kuwa imara tena,” akitumia kauli mbiu kama ile ya kampeni ya Trump “Kuifanya Marekani kuwa imara tena.”

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema makubaliano ya Paris ni “hatua kabambe ya kihistoria.’

Aliongeza kusema kuwa “Uamuzi huo hauwezi wala hautaweza kuwazuia wale wenzetu ambao wanahisi wanajukumu la kuilinda dunia kuendelea na juhudi hizo.

"Nasema wale wote ambao mustakbali wa dunia yetu ni muhimu kwao: Basi tuendelee katika njia ya kushikamana pamoja ili tuweze kufanikiwa kuilinda dunia."

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post