Forbes: Wasanii na wachezaji matajiri zaidi duniani 2017


Beyonce na JK Rowling ndio wanawake pekee katika 10 waliopata pesa nyingi zaidi

Jarida la Forbes limetoa orodha ya watumbuizaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi duniani, Sean "Diddy" Combs ndiye anayeongoza.

Mapato yake yalikuwa $130m (£102m), jambo lililomsaidia kupanda sana kutoka nafasi ya 22 mwaka jana.

Ufanisi wake unatokana na ziara yake ya majuzi Marekani, mkataba wa mauzo kati yake na kampuni ya vodka na hatua yake ya kuuza nembo yake ya mavazi ya Sean John.

Beyonce na JK Rowling wanashikilia nafasi ya pili na ya tatu mtawalia, lakini jambo la kushangaza ni kuwa wanawake katika orodha hiyo ya wasanii na wachezaji 100 ni asilimia 16 pekee.

Walioingia katika orodha hiyo mara ya kwanza mwaka huu ni pamoja na Kylie Jenner, aliye nafasi ya 59.

Yeye ndiye wa umri mdogo zaidi katika orodha hiyo, akiwa na miaka 19.

Mapato yake yanatokana sana na kipindi cha uigizaji wa maisha ya uhalisi runingani cha familia yake, kipindi cha Keeping Up with the Kardashians. Alipokea mapato pia kutoka kwa kampuni ya manukato na vipodozi ambayo ina jina lake, nembo ya mavazi na pia kushirikishwa katika kutangaza na kuuza bidhaa mbalimbali.

Nusu ya walio katika 10 bora ni wanamuziki, lakini kuna wachezaji wawili - Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na nyota wa mpira wa kikapu LeBron James.

Hii hapa orodha ya 10 bora:
1. Sean "Diddy" Combs - $130m (£102m)Combs alijipatia jumla ya $70m baada ya kuuza theluthi ya biashara yake ya mavazi

Combs, mwanamuziki mshindi wa Grammy, alifahamika sana kwa albamu zake maarufu kama vile No Way Out and Forever. Lakini biashara zake za ujasiriamali pia zimemuongezea utajiri, aliruka kutoka nambari 22 mwaka jana na kuongoza mwaka huu.
2. Beyonce Knowles - $105m (£82.7m)Nyota huyu kwa sasa ana mimba ya pacha

Malkia Bey hahitaji kutambulishwa. Nyimbo zake zimekuwa juu kwenye chati na amepanda kutoka nambari 34 mwaka jana. Mapato yake sana ni kutokana na ziara yake ya kimuziki ya Formation na albamu aliyoichomoa karibuni, ya Lemonade. Mumewe, Jay-Z, alifanikiwa tu kufika nambari 55.
Vijana 10 matajiri zaidi duniani
3. JK Rowling - $95m (£74.8m)Rowling majuzi amemaliza kuandika hadithi ya filamu ijayo ya Fantastic Beasts

JK Rowling amerejea katika 100, sana kutokana na mchezo wake wa kuigiza wa sehemu mbili , Harry Potter na Cursed Child na pia filamu za Fantastic Beasts na Where to Find Them.
4. Drake - $94m (£74.06m)Mwanamuziki huyu kutoka Canadian alijishindia tuzo kadha mwezi jana

Nyota hutu wa hip hop kutoka Canada aliruka kutoka nambari 69 mwaka jana hadi nambari nne, baada ya kuongeza mara dufu mapato yake sana kupitia ziara ya kimuziki na kupewa mikataba za kutangaza bidhaa za kampuni kama vile Nike, Sprite na Apple.
5. Cristiano Ronaldo - $93m (£73.2m)Ronaldo amefunga mabao katika fainali tatu tofauti Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

Mchezaji nyota huyu wa Real Madrid ameshuka nafasi moja mwaka huu. Kando na mapato kutoka kwa soka, mchezaji huyu bora duniani wa Fifa pia alijizolea pesa kutoka kwa mauzo ya mavazi yenye nembo yake yakiwemo suruali za ndani na jeans, pamoja na mkataba wake na Nike.
6. The Weeknd - $92m (£72.45m)Nyota The Weeknd akiwa na mpenzi wake Selena Gomez at the Met Ball

Mwanamuziki mwingine kutoka Canada, The Weeknd, ameingia kwenye 10 bora kwa mara ya kwanza, baada ya kufika 30 bora mwaka jana.

Albamu yake ya karibuni zaidi, Starboy, iliibuka ya tatu kwa mauzo wiki ya kwanza Marekani mwaka 2016.

Majuzi alishirikiana na Lana Del Ray katika wimbo Lust for Life.
7. Howard Stern - $90m (£70.86m)Howard Stern amekuwa akiandamwa an utata

Msanii huyu aliyejipatia hadhi ya kuwa "mfalme wa vyombo vyote vya habari" ameendelea kushikilia nafasi ya saba aliyokuwa nayo mwaka jana.

Jaji huyu wa zamani wa America's Got Talent kwa sasa ana mkataba wa miaka mitano na Sirius XM Radio.
8. Coldplay - $88m (£69.33m)Coldplay majuzi aliigiza katika tamasha la One Love Manchester

Coldplay wamerejea kwenye orodha hii baada ya kufanikiwa kwa ziara yao ya kimuziki waliyoipatia jina Head Full of Dreams, ambayo ilimalizikia Australia na New ZealandDesemba. Ni habari njema kwa wanaotoa msaada wka hisani, kwani bendi hiyo hutoa asilimia 10 ya faida yao kwa hisani.
9. James Patterson - $87m (£68.53m)Patterson amefurahia mauzo ya vitabu vyake mtandaoni

Kuna mwandishi mwingine orodha hii - Patterson ambaye amechapisha vitabu zaidi ya 130 na anaaminika kuwa mwandishi vitabu aliyeuza vitabu vingi zaidi ambaye bado yuko hai.

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton kwa sasa anaandika kitabu kuhusu White House kwa ushirikiano naye.
10. LeBron James - $86m (£67.8m)LeBron ni nyota mkubwa sana US

Mchezaji huyu nyota wa mpira wa kikapu anayechezea Cleveland Cavaliers alilipwa mshahara wa jumla ya $31m (£24.4m) 2016-17.

Hilo lilimfanya kuwa mchezaji wa tatu pekee wa NBA kulipwa $30m msimu mmoja baada ya Michael Jordan na Kobe Bryant.

Pia, hushirikishwa kuudha bidhaa za kampuni kama vile Nike, Coca-Cola na Beats ya Dre.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post