Bravo alikua nyota wa mchezo
Chile imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la mabara baada ya kuondosha Ureno kwa penalti 3-0.
Mlinda mlango wa Manchester City Claudio Bravo alikua shujaa wakati timu yake ya Chile ilipoiondosha Ureno katika hatua ya nusu fainali na kutinga fainali.
Chile imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la mabara baada ya kuondosha Ureno kwa penalti 3-0.
Bravo aliokoa mikwaju ya penalti iliyopigwa na Ricardo Quaresma, Joao Moutinho na Nani huku Chile wakifanikiwa kupata penalti tatu.Image captionMra ya mwisho Bravo kuokoa mkwaju wa penalti ilikua Oktoba dhidi ya Tottenham
Ilikuwa bahati nzuri kwa Chile kwani mlinda mlango wao alionekana makini zaidi na kujiamini kitendo cha kuweza kuokoa mikwaju yote mitatu.
Chile itamenyana na Ujerumani ama Mexico katika fainali siku ya Jumapili katika mji wa St Petersburg.
Post a Comment