Najua
utakua umesikia mara nyingi kuhusu wanasayansi na watafiti wa masuala
ya anga wakitoa taarifa mbalimbali kuhusu kilichopo kwenye Sayari
nyingine ukiacha Dunia.
Leo April 12, 2017 Nakusogezea mambo 6 muhimu
ya kufahamu kuhusu jinsi ilivyo Sayari ya Venus ambayo ipo jirani na
ukubwa wake unafanana na dunia ila tu ina mazingira tofauti na ni
hatari.
Kwa mujibuwa shirika la utafiti wa masuala ya anga la nchini Marekani NASA, nimeyapata mambo 6 kuhusu Sayari ya Venus.
- Sayari ya Venus ina unga sumaku mdogo kuliko dunia. Inaelezwa kuwa uchache wa ungasumaku husababisha mionzi ya anga ya jua kuingia kwenye angahewa, na mionzi hiyo huzalisha umeme kutokea kwenye mawingu.
- Venus ina volkano nyingi zaidi kuliko sayari nyingine yoyote ya mfumo wa jua. Wanasayansi wamegundua aina za volkano 1600 kwenye sayari hiyo.
- Venus ikizunguka yenyewe kwa mzunguko mmoja inahitaji siku 243 za dunia, na ikizunguka jua kwa mzunguko mmoja inahitaji siku 224.7 kwenye dunia. Unaona sentensi hii ni ngumu kuielewa? Hii inamaanisha kuwa kwenye sayari hiyo siku moja ni ndefu zaidi kuliko mwaka mmoja!
- Asilimia kubwa ya hewa kwenye Venus ni Carbon Dioxide, ambayo inasababisha sayari hiyo kuwa na joto kali, ambalo kuna wakati hufikia nyuzijoto 470 sentigredi.
- Mgandamizo wa hewa kwenye Venus ni mkubwa mara 90 ya ule wa dunia, na karibu sawa na mgandamizo wa maji kwenye kina cha kilomita 1 chini ya bahari.
- Venus ni sayari yenye vimbunga vingi. Mwendokasi wa upepo wa sayari hiyo unaweza kufikia kilomita 724 kwa saa, ambao ni mkubwa zaidi kuliko mwendokasi wa kimbunga kikubwa zaidi duniani.
Post a Comment